Balozi
wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini Mheshimiwa Lu Younqing
(Kushoto) alipokutana na Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli (katikati) katika Ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Ujenzi,
jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi
Herbert E. Mrango.
Jamhuri
ya Watu wa China imeendelea kuelezea dhamira yake ya kukuza ushirikiano
na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hususan katika sekta ya ujenzi.
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini Mheshimiwa Lu Younqing
amefanya mazunumzo na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli alipomtembelea ofisini kwake na kubainisha azma hiyo ya kukuza
ushirikiano kati ya nchi mbili hizi.
Miradi
mingi mikubwa ya ujenzi hapa nchini imekuwa ikitekelezwa na makandarasi
kutoka China. Makampuni hayo yamejikita zaidi katika maeneo ya ujenzi
wa barabara, majengo makubwa, miradi ya maji, kilimo pamoja na
miundombinu ya mawasiliano.
Waziri
wa Ujenzi akimshukuru Balozi huyo kwa kumtembelea, amezipongeza kampuni
za Kichina ambazo zinatekeleza miradi ya ujenzi wa barabara, madaraja
na majengo hapa nchhini kwa kuzitekeleza kazi hizo kwa ubora unaoendana
na viwango vilivyowekwa lakini kwa gharama nafuu. Hata hivyo, Waziri
Magufuli aliezea kuwepo kwa baadhi ya kampuni za Kichina ambazo utendaji
wake hauridhishi kwamba Wizara yake haitasita kuzichukulia hatua kali
za kisheria na amemuomba Mheshimiwa Balozi Younqing kushirikiana naye
katika kuwafuatilia makandarasi wote watakaoanza kulichafua jina zuri
ambalo linaendelea kujengaka kwa makampuni ya ujenzi kutoka China.
Naye,
Balozi Younqing akimhakikishia ushirikiano Waziri wa Ujenzi, pia
amemuarifu kwamba tayari maelekezo yametolewa kwa makandarasi wote wa
Kichina wanaofanya shughuli zao hapa Tanzania kuhakikisha kuwa pale
inapowezekana wanatumia bidhaa na mali ghafi zinazopatikana hapa nchini
ikiwa ni pamoja na Wataalamu wa Kizalendo.
Post a Comment