Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampauni ya Bia Tanzania (TBL) Robin Goetzsche (wa tatu
kushoto) akikabidhi funguo kama ishara ya kukabidhi basi la Taifa Stars
kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Leodgar Tenga (wan ne
kushoto) wakati Kilimanjaro Premium Lager ilipokabidhii basi hilo jana
makao makuu ya TBL Jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kaviske, Mkurugenzi
wa Masoko wa TBL Kushilla Thomas, Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen,
Mchezaji wa Taifa Stars aliyewawakilisha wenzake, Erasto Nyoni, Katibu
Mkuu wa TFF Angetile Osiah, Ofisa Mwandamizi wa Baraza la Michezo
Tanzania, Chalukulu John na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Sunday Kayuni.
(Picha na mpiga picha wetu).
Kocha
wa Timu ya Taifa Kim Poulsen akishuka kutoka kwenye basi jipya la Taifa
Stars lililolabidhiwa na Kilimanjaro Premium Lager.
Pichani
juu na chini ni Washangiliaji mbalimbali wa Taifa Stars wakati
Kilimanjaro Premium Lager ilipokabidhi basi jipya kwa Taifa Starsaifa
katika makao makuu ya TBL Ilala jana.
Kampuni
ya Bia Tanzania Limited kupitia bia yake ya Kilimanjaro, leo hii
imekabidhi basi jipya kwa Timu ya Taifa (Taifa Stars), likiwa na thamani
ya zaidi ya Sh milioni 200 kwa udhamini wa Bia ya Kilimanjaro Premium
Lager.
Hafla
ya makabidhiano imefanyika Makao Makuu ya TBL jijini Dar es Salaam na
kupewa Baraka na Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robin Goetzsche. Hafla hiyo pia
ilihudhuriwa na maofisa kutoka TFF, wafanyakazi za TBL, wadau wa soka
na vyombo mbalimbali vya habari.
TBL
imenunua basi hilo ikiwa ni sehemu ya ufadhili kama ilivyoanishwa
katika mkataba baina ya pande hizo mbili. Mkataba huo ulitiwa saini Mei
mwaka jana na lengo kuu ni kuinua kiwango cha Taifa Stars.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TBL alisema: Imeshatimia miezi 10
tangu tuanze kuifadhili Taifa Stars na malengo yetu kama wadhamini ni
kuiona timu ikipata ushindi uwanjani ma hivyo kuongeza sifa ya timu na
tumeridhika na matokeo.”
Mkurugenzi
huyo alisema, kukabidhi kwa basi hilo ni ishara kwamba TBL itaendelea
kuisadia timu ya taifa na hivyo kupandisha kiwango cha soka nchini na
aliwataka wahusika kulitunza basi hilo kwa manufaa ya timu na taifa kwa
ujumla. “Tutaendelea kutoa msaada na tunatarajia kuwa nanyi kwa nafasi
yenu mtafanya bidii na hivyo kutupa moyo wa kuendelea na uwekezaji.
Tunaamini mtafanya vizuri katika mechi nyingi za kimataifa na hivyo
kupanda kwenye viwango vya FIFA.”
Kwa
upande wake, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema basi
hilo lenye uwezo wa kubeba abiria 51, limenunuliwa kutoka Yutong na
thamani yake ni zaidi ya Sh milioni 200.
Akitoa
ufafanuzi, Kavishe alisema basi hilo kutoka Kampuni ya Yutong lina
Chassis ya 4X2, uwezo wa injini ni 300 HP Cummins, huku likiwa na uwezo
wa kumeza lita 800 za mafuta. Mbali na hayo kila siti ina mkanda wa
abiria kwa ajili ya usalama wakati wa safari, luninga mbili, redio yenye
spika nane, mafriji mawili, viyoyozi na milango ya kisasa inayojifungua
na pia nafasi kutoka kiti kimoja hadi kingine ni kubwa.
“Wachezaji
wetu lazima wawe na nafasi nzuri ya kupumzika wakati wa safari, na hiyo
ndiyo sababu iliyotufanya tumumue basi hili la kisasa zaidi likiwa na
vifaa muhimu ambavyo pia ni vya kisasa…tunawaomba kulitunza basi hili,”
alisema Kavishe na kuongeza kuwa ni jukumu lao kufanya hayo kwa mujibu
wa mkataba ili kuinua kiwango cha timu.
Baada
ya makabidhiano hayo, basi lilifanya ziara katika maeneo mbalimbali ya
Dar es Salaam ili mashabiki walione na kupiga picha huku kukiwa na
matukio kadhaa ya kusisimua kama vile kucheza na kuimba.
Naye
Rais wa TFF, Leodgar Tenga aliipongeza TBL kwa udhamini wake wa uhakika
na kusisitiz akuwa tangu wameanza wameshatekeleza ahadi walizoahidi na
moja wapo ikiwa ni kuhakikisha basi jipya linanunuliwa.
“Hawajawahi kuchelewesha malipo hata mara moja na kwa hilo tunawashukuru sana,” alisema Rais Tenga.
Bia
ya Kilimanjaro ilianza kuifadhili Taifa Stars Mei mwaka jana kwa
mkataba uliogharimu zaidi ya Sh bilioni 2 kwa mwaka katika kipindi cha
miaka mitano na TFF.
Post a Comment