Waziri Mkuu mstaafu,
Cleopa Msuya, aliyekuwa amelazwa katika Taasisi ya Mifupa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MOI), amepelekwa nchini Uingereza kwa matibabu zaidi. Afisa Habari wa
Taasisi hiyo, Jumaa Almasi, alisema jana kuwa Mzee Msuya aliondolewa MOI juzi
saa 3:00 usiku. “Serikali imeamua kumpeleka Mzee Msuya nchini Uingereza kwa
ajili ya matibabu zaidi, na aliondolewa hospitalini hapa jana (juzi) usiku,”
alisema Almasi. Hata hivyo, bado haijaeleweka ugonjwa unaomsumbua kiongozi huyo
mstaafu. Serikali na Moi hawakuwa tayari kuzungumzia igonjwa
unaomsumbua.
Chanzo chetu jana
ilimtafuta Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, DK Hussein Mwinyi, ambaye licha ya
kuthibitisha kuwa na taarifa za kupelekwa nchini Uingereza kwa Mzee Msuya,
lakini hakutaka kuweka wazi ugonjwa unaomsumbua.
Mzee Msuya alilazwa kitengo
cha mifupa tangu Jumatatu wiki hii na kuwekwa chini ya uangalizi wa jopo la
madaktari wa taasisi hiyo pamoja na wenzao wa Muhimbili, ambao walikuwa
wanamfanyia uchunguzi wa afya yake na ilielezwa kuwa hali yake ilikuwa
inaendelea vizuri.
Mzee Msuya alikuwa Waziri Mkuu kwenye uongozi wa awamu ya
kwanza ya Hayati Mwalimu Jullius Nyerere, na awamu ya pili ya Rais Ali Hassan
Mwinyi .
Chanzo chetu jana ilimtafuta Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, DK Hussein Mwinyi, ambaye licha ya kuthibitisha kuwa na taarifa za kupelekwa nchini Uingereza kwa Mzee Msuya, lakini hakutaka kuweka wazi ugonjwa unaomsumbua.
Mzee Msuya alilazwa kitengo cha mifupa tangu Jumatatu wiki hii na kuwekwa chini ya uangalizi wa jopo la madaktari wa taasisi hiyo pamoja na wenzao wa Muhimbili, ambao walikuwa wanamfanyia uchunguzi wa afya yake na ilielezwa kuwa hali yake ilikuwa inaendelea vizuri.
Mzee Msuya alikuwa Waziri Mkuu kwenye uongozi wa awamu ya kwanza ya Hayati Mwalimu Jullius Nyerere, na awamu ya pili ya Rais Ali Hassan Mwinyi .
Post a Comment