Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Dr. Nchimbi: Kuuwawa kwa Padri huko Zanzibar si Ujambazi bali ni Ugaidi!



PADRI wa kanisa katoliki jimbo la Zanzibar,amepigwa risasi za kichwa na kifuani na kuuwawa na watu wasiojulikana.

Padri huyo aliyetambuliwa kwa jina la Evaritus Gabriel Mushi wa kanisa katoliki parokia ya mtakatifu Joseph Shangani mjini , Zanzibar

Watu hao ,ambao hawajafahamika wala kukamatwa ,walifanya unyama huo jana saa 12 Alfajiri asubuhi nje ya kigango cha mtakatifu theresia kanisa la mtoni,wakati akijiandaa kushuka kwenye gari kuingia kanisani kufanya maandalizi ya ibada ya jumapili.

Akizungumza na waandishi wa habari kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa Alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Alisema kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maafisa wa jeshi hilo Padri Mushi ,alipigwa risasi akiwa kwenye ndani ya gari na kujeruhiwa vibaya sehemu za kichwa na kifua.
Alisema baada ya kutokea kwa tukio hilo punde baadhi ya waumini wa kanisa hilo waliofika katika kanisa hilo kwa ajili ya ibada walimpeleka Padri Mushi katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja kwa ajili ya matibabu baada ya muda mchache Akafariki dunia.

“Kutokana na uzito wa tukio hili jeshi la polisi Zanzibar linaendelea na upelelezi wa kina kuhakikisha wahusika wote wanafikishwa katika vyombo vya kisheria.”Alisema kamishna Mussa

“Natoa wito kwa wananchi washirikiane na maafisa wetu juu ya taarifa zozote zinazohusiana na tukio hili ili tuweze kutekeleza majukumu kwa wakati.” Aliendelea kusisitiza



Kamanda wa polisi mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ,ACP Aziz Mohamed alisema kwa sasa jeshi la polisi linaendelea na doria katika maeneo mbalimbali ya Mjini wa Zanzibar ili kuhakikisha wale wote wanaohusika katika mauaji ya padri huyo wanakamatwa.

Wakati huo huo ,Naye Mkuu wa Mkoa Mjini Magharib Abdallah Mwinyi Amefika katika Viunga vya Hospitali ya Mnazi Mmoja Mnamo wa Saa 4 Asubuhi kwa ajili ya kuwafariji Jamaa,ndugu na waumini wa dini hiyo waliofika katika eneo hilo kwa ajili ya kufuatilia hatima ya kiongozi wao.

Akizungumzia tukio hilo,msemaji wa kanisa hilo ambaye pia ni katibu mkuu wa kanisa katoliki,jimbo la Zanzibar padri Cosmas Shayo aliwataka waumini wa kanisa hilo,kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki hadi suala hilo litakapotafutiwa ufumbuzi.

Alisema Uongozi wa kanisa hilo,umepokea suala hilo kwa masikitiko makubwa pia kufariki kwa padri huyo ni miongoni mwa pigo kubwa kwa waumini na kanisa kwa ujumla.

“Tukio hili si la kufumbia macho kwani viongozi na waumini wa kanisa katoliki Zanzibar kwasasa tunaishi kwa mashaka hali ya kuwa,mtu ukitoka asubuhi huna uhakika wa kurudi jioni ukiwa hai”Alisema padri Shayo.

“Kwa nini matukio haya yanaandama waumini na viongozi wa kanisa katoliki hapa kuna agenda ya siri hadi tunafikia hatua ya kuishi kama watumwa tukiwa na hofu juu ya usalama wa maisha yetu,serikali na vyombo vya ulinzi vikiwa vinakaa kimya.”Aliendelea kusema Padri shayo.


Alisema Kanisa linathamini mchango mkubwa uliotolewa na marehemu wakati wa uhai wake,katika kuliendeleza kanisa kwenye huduma za kiimani na kiroho kwa waumini wa kanisa.

Baadhi ya mashuhuda ,waliozungumza kwa nyakati tofauti katika eneo la tukio ambapo walisema kwamba walifika mapema katika Kanisa hilo kwa ajili ya maandalizi ya ibada,pembeni mwa kanisa hilo kulikuwa na watu watatu ambao hawakujulikana kwa haraka ghafla baada ya kufika padri Mushi walisikia milio ya risasi wawili wakaondoka mbio na pikipiki aina ya vespa na mmoja akatokomea Vichochoroni.

Wananchi wamesikika wakitupia lawama jeshi la polisi kwa kushindwa kudhibiti uharifu na umiliki wa silaha kinyume cha sheria,kwani matukio ya kushambuliwa kwa viongozi wa dini mbalimbali Zanzibar yameshamili.
Wakati huo huo ,Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt, Emmanuel Nchimbi amesema serikali itahakikisha inafanya juhudi kuhakikisha inawakamata watu waliomuua Padre Evarist Mushi wa kanisa katoliki Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Makao makuu ya Polisi Zanzibar Dkt, Nchimbi amesema serikali imesikitishwa na tukio hilo alilolieleza kuwa ni la kigaidi huku akishtumu kuwa wana lengo la kuingiza nchi katika machafuko.

Amesema kuwa tukio hilo si tukio la ujambazi bali tukio la kigaidi kwani limelenga zaidi katika kuwashambulia viongozi kidini.
Amesema kuwa tukio hili limefanana na tukio lililotokea mwishoni mwa mwaka jana la kushambuliwa kwa risasi Padre Ambrose Mkenda wa Kanisa katoliki parokia ya Mpendae.
Amesema kuwa katika kukabiliana na matukio ya kihalifu hapa nchini Wizara imeomba kibali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushirikia na mashirika ya kimataifa ya upelelezi ili kuwakamata wahyalifu hao.


Waumini wa Dini ya Kikiristo wakiwa katika Hospitali ya Mnazi kufuatia tukio lililotokea.

Dkt, Nchimbi amewataka Watanzania kuwa wavumilivu na kujiepusha katika mtego wa kuchukia na kwa misingi ya kidini katika kipindi hichi ambacho Jeshila Polisi linaendelea na upelelezi wa tukio hilo.
Padre Evaristus Mushi ameuwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana ambao walikua wamepanda pikipiki aina ya Vespa leo asubuhi wakati akielekea kuongoza misa katika kanisa la Mtakatifu Theresia la Beit el Rass.


Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top