Naibu meya wa Manispaa ya Iringa Gravas
Ndaki akishangaa ajali ya karne yenye maajabu makubwa kwa mkoa wa
Iringa ,ajali iliyotokea usiku wa leo eneo la Hoteli ya kati (makosa)
au CRDB ya zamani katika barabara ya Iringa -Dodoma,hakuna majeruhi
wala aliyepoteza maisha
Askari wa usalama barabara nao washangaa kuona ajali kama hii katikati ya mji
Mmiliki wa gari aina ya RAV 4 iliyogonga gari na kulipanda juu akiwa haamini kilichotokea
Huyu ndie mmiliki wa RAV4 inasadikika ni mfanyakazi wa Tanroads mkoa wa Iringa
Dereva wa Taxi yenye namba za usajili T 510 AYUKelvin Kaduma akiwa salama kabisa
Hii ni ajali ya pili kutokea usiku wa
leo katika Manispaa ya Iringa imetokea eneo la Kitwiru baada ya lori
lililobeba mbao kuacha njia na kugonga nguzo ya umeme kabla ya kuanguka
,hakuna aliyepoteza maisha wala majeraha ya kutisha
Hii ni nguzo ya umeme na kibanda kilichogongwa na lori hilo
Shehena ya mbao zikiwa zimemwagika baada ya ajali hii
imechotwa: Audiface Blog
Post a Comment