SIKU MOJA baada ya Mfuko wa
Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kuwatembezea wadau na wanachama
wake katika nyumba za mradi wa nyumba za makazi ambazo zimejengwa na
Shirika hilo eneo la Buyuni kata ya Majohe Chanika Wilayani Ilala nje
kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo
Mbene nae ametembelea na kujionea nyumba hizo na kuumwagia sifa Mfuko
huo kwa ubunifu na kuwajali wananchama wake.
Mbene pia alitembelea Ujenzi wa jingo la Kitegauchumi la Ghorofa 35 linalojengwa na Mfuko huo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu akimpa maelezo
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene juu ya muundo kamili wa
Jengo hilo la ghorofa 35 ambalo linajengwa na PSPF jijini Dar es Salaam
na litakuwa na maduka, makazi na Ofisi.
Meneja
Mradi wa Ujenzi wa Jengo hilo la PSPF Tower, Ghazi Al Shamali (kushoto)
akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa
Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu juu ya hatua zilizofikiwa
hadi sasa katika ujenzi huo.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet
Zebedayo Mbene akiangalia thamani za ndani katika moja ya vyumba katika
nyumba zilizopo ndani ya jengo hilo la PSPF Tower ambalo ujenzi wake
bado unaendelea na pindi zitakapo kamilika zitauzwa kwa watumishi wa
Serikali pamoja na Wanachama wa Mfuko huo.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet
Zebedayo Mbene na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa
Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu wakiongozana kuteremka
ngazi zilizopo katika moja ya nyumba (apartment) zilizopo katika jingo
hilo la PSPF Tower ambalo linaendelea kujengwa.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet
Zebedayo Mbene akitembezwa ndani ya jengo hilo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu.
Watumishi wa PSPF wakizungumza jambo ndani ya Jengo hilo.
Awali Naibu Waziri wa Fedha, Janet
Zebedayo Mbene alipata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba
491 za Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) zinazojengwa
Buyuni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na ambazo zimekamilika ujenzi
wake na kuanza kuuzwa kwa Wanachama wa mfukjo huo. Pichani mbele kutoka
kushoto ni Gabriel Silayo,
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PSPF, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene na Mkurugenzi wa Fedha wa PSPF, Masha Mshomba wakimtembeza Kiongozi huyo katika nyumba hizo.
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PSPF, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene na Mkurugenzi wa Fedha wa PSPF, Masha Mshomba wakimtembeza Kiongozi huyo katika nyumba hizo.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene akiwa na Mkurugenzi wa Fedha wa PSPF, Masha Mshomba akimtembeza ndani ya moja ya nyumba hizo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF,
Adam Mayingu akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene nje
ya moja ya nyumba ambazo zimejengwa na PSPF, kwaajili ya kuwauzia
wanachama wake kwa gharama nafuu.
Post a Comment