Halmashauri Kuu ya
Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi itafanya Mkutano wake wa kawaida kuanzia
tarehe 10 -11 /02/2013. Kikao hicho kitaongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM,
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
Wajumbe wa NEC
wanatarajiwa kufika Mjini Dodoma leo tarehe 9/02/2013,kwa ajili ya kikao hicho.
Pamoja na mambo
mengine kikao hichi kitatanguliwa na Semina ya siku mbili kwa Wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa.
Lengo la Semina hii
ni kuwaongezea Wajumbe uelewa kuhusu masuala ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali
yake hasa ikizingatiwa kwamba wengi wa Wajumbe ni wapya kufuatia Uchaguzi Mkuu
wa CCM wa mwaka 2012.
Mada
zitakazowasilishwa kwenye Semina ni pamoja na;
1. Nafasi na Wajibu
wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
2. Umuhimu wa Maadili
kwa Viongozi na Watendaji wa Chama Cha Mapinduzi.
3. Mikakati ya
kutekeleza maazimio ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa nane wa CCM.
4. Mkakati wa kukuza
ajira nchini.
Semina hii itafuatiwa
na Mkutano rasmi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ambao pamoja na mambo mengine
utafanya Uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha
Mapinduzi.
Imetolewa:
Nape Moses Nnauye
KATIBU WA NEC –
ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA
MAPINDUZI
Post a Comment