Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAAFISA HABARI WATEMBELEA BUNGE, UDOM NA KUPANDA MITI


 

Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Habari Bw. Raphael Hokororo akiwafundisha maafisa habari na mawasiliano wa serikali kutoka Wizara, Taasisi, wakala, mashirika ya Umma, mikoa na wilaya upigaji wa picha bora za mnato kwa matumizi ya habari wakati wa kuhitimisha kikao cha maafisa hao mjini Dodoma.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana ambaye alikua miongoni mwa waalikwa waliohudhuria kikao kazi cha maafisa habari na mawasiliano wa serikali akiongea na mafiasa hao mjini Dodoma.
Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma kufuatia mwaliko wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara.
Maafisa habari na mawasiliano wa serikali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Baadhi ya viongozi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Mkurugenzi wa Idara hiyo Bw. Assah Mwambene (wa nne kutoka kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Usajili wa Magazeti Bw. Raphael Hokororo (wa pili kutoka kushoto) wakiwa wamesimama ndani ya ukumbi wa Bunge kuwasalimia waheshimiwa wabunge mara baada ya kuombwa na Mh. Spika wakiwaongoza maafisa habari wa serikali.
Maafisa Habari na Mawasiliano wa serikali wakiwasili Chuo Kikuu cha Dodoma kushiriki zoezi la upandaji wa miti chuoni hapo ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kuhifadhi mazingira ya chuo hicho.
Mhasibu mkuu msaidizi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Swalehe Chondoma akishiriki zoezi la upandaji wa miti katika kampasi ya chuo kikuu cha Dodoma.
Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akizindua zoezi la upandaji wa miti lililowahusisha mafisa habari wa Serikali katika kampasi ya chuo kikuu Dodoma.
Maafisa habari na Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na zoezi hilo Chuo kikuu cha Dodoma.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.



habaa2 63f39

Cecilia korassa, Afisa Uhusiano wa mamlaka ya bandari, Tanga akipanda mti chuoni hapo

Maafisa wa habari, mawasiliano na uhusiano wa serikali ambao wapo mjini Dodoma kwa ajili ya kikao kazi kinachoendelea, Juzi walitembea Chuo Kikuu cha Dodoma wakiwa chuoni hapo maafisa hao walipata fursa ya kupanda ikiwa ni ishara ya kuhamasisha umma katika kutunza na kuhifadhi mazingira

habaa 1 4520f

habaa 69dc6

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top