Kaimu kamanda wa polisi
mkoa wa mara japhet lusingu akitoa taarifa kwa vyombo vya
habari.
MAUAJI ya kikatili kwa
wanawake mkoani Mara, yameendelea kushika kasi ambapo wanawake watatu wameuawa
katika matukio yaliyotokea mfululizo kwa siku moja.
Kaimu Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mara, Japhet Lusingu, alisema katika tukio la kwanza, mkazi wa Kijiji
cha Tonyo, Kata ya Bisumwa wilayani Butiama, Happyness Lucas (25) alifariki
dunia Februari 11, 2013 baada ya kujeruhiwa kwa kupigwa teke tumboni na mume
wake, Rugera John (27).
Chanzo cha ugomvi huo kilichosababisha kifo cha Happyness ni kugombea kandambili ambazo mume wa marehemu alikuwa amemnunulia mke mdogo.
Alisema baada ya kupigwa alipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Butiama kwa matibabu, ambapo saa tano usiku alifikwa na mauti.
Katika tukio jingine, alisema lilihusisha kifo cha mkazi wa Mtaa wa Chiringe wilayani Bunda, Rhobi Lucas (24), kilichotokea Februari 11, 2013 baada ya kushambuliwa na kupigwa mateke na mumewe, Masumbuko Khamis.
Alisema Januari 28, saa tatu usiku, Masumbuko alifika nyumbani kwake akiwa ameongozana na hawara yake na kuanzisha ugomvi baina yake na mkewe Rhobi, ambapo walianza kumshambulia marehemu kwa kushirikiana na mpenzi wake mwingine.

Post a Comment