Walimu wote waliopewa ajira
ya Ualimu Serikalini ambao majina yao yametangazwa katika tovuti za Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI, wanatakiwa
kuripoti tarehe 01 Machi 2013 kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri
walikopangiwa kwa ajili ya kupangiwa Vituo vya kazi. HAKUNA MABADILIKO YA VITUO
VYA KAZI YATAKAYOFANYWA. Mwalimu anatakiwa kwenda na vyeti vyake halisi vya
taaluma na cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala zake. Mwalimu ambaye hataripoti
ifikapo tarehe 9 Machi 2013 atapoteza nafasi hiyo.
NB: WALIMU WALIOKWISHA AJIRIWA WARUDI KWA WAAJIRI WAO
http://www.moe.go.tz
AJIRA MPYA YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI MWAKA 2012/13 (1006.83 kB)
Post a Comment