Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
akizungumza na waaandishi wa habari juu ya Tamko la Halmashauri Kuu ya Taifa ya
CCM,katika ukumbi wa Sekretarieti, mjini Dodoma.Picha zote na Adam Mzee-idara ya
itikadi na Uenezi-CCM
--
1.
Halmashauri Kuu ya Taifa imepokea maelezo ya Serikali kuhusu
maandamano na vurugu zilizotokea Mkoani Mtwara tarehe 27 Desemba, 2012 tarehe 25
Januari, 2013 na tarehe 26 Januari, 2013. Maandamano na vurugu hizo zilizodaiwa
kuwa na lengo la kupinga mradi wa bomba la Gesi kujengwa na kupeleka Gesi Dar es
Salaam.
2. Baada ya
kupokea maelezo haya ya Serikali, Halmashauri Kuu ya Taifa imebaini kuwa:
-
(a)
Kwa sehemu kubwa Wananchi wa Mkoa wa Mtwara hawakuwa wamepewa
elimu ya kutosha juu ya uendelezaji wa Gesi na jinsi
watakavyonufaika.
(b)
Baadhi ya Wanasiasa na baadhi ya Viongozi wa Makundi mbalimbali
waliamua kutomia suala la Gesi kupandikiza lugha za chuki, uchochezi na
upotoshaji wa maendeleo ya Mradi wa Gesi kwa lengo la kujitafutia
umaarufu.
(c)
Suala la Gesi limetumika kama kisingizio tu cha kufanya vitendo
vya rurugu na uvunjifu wa amani.
3. Kutokana na ukweli huu,
Halmashauri Kuu ya Taifa inaelekeza ifuatavyo:-
(i)
Imesikitishwa na vurugu zilizotokea na kusababisha watu kadhaa
kupoteza maisha na uharibifu mkubwa wa mali na majengo
ya CCM, Serikali, Wabunge na watu binafsi. Halmashauri Kuu ya Taifa
inawapa pole wafiwa na waliopoteza mali zao.
(ii)
Inaiagiza Serikali kufanya uchunguzi wa kina kuhusu waliofanya vurugu na
uharibifu mbalimbali na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa Sheria. Pia, kuwa
makini na kuhakikisha matukio kama haya hayajitokezi tena.
(iii)
Inaiagiza Serikali kuendelea kutoa elimu ya kutosha kwa Wananchi
wa maeneo husika kuhusishwa na kuelimishwa juu ya miradi
mbalimbali kwenye maeneo yao.
(iv)
Halmashauri Kuu ya Taifa inawataka Wananchi wa Mkoa wa Mtwara
kuendelea kuishi kwa amani na utulivu kama ilivyo desturi yao, maana vurugu
pamoja na kuharibu mali na kugharimu maisha vinaweza kuwakimbiza
wawekezaji waliojitokeza na ambao shughuli zao
zitawafaidisha wananchi wa Mkoa huu na Watanzania kwa ujumla
.
HALMASHAURI KUU YA
TAIFA
Dodoma 10 – 11
Februari,2013
Post a Comment