Mwenyekiti wa kamati ya
uwasilishaji wa mapendekezo ya muundo wa mabaraza ya Katiba kwa jamii ya watu
wenye ulemavu, Bw. David Nyendo (kushoto) akiwasilisha maoni yake ya kamati hiyo
kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano baina yao uliofanyika leo
(jumatano Feb. 13, 2013) katika ofisi za makao makuu ya Tume Jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Mjumbe wa Tume, Dkt. Salim Ahmed Salim.
Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia) akizungumza na wawakilishi wa
makundi ya jamii ya watu wenye ulemavu ukiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo,
Bw. David Nyendo (kushoto) mara baada ya kufika katika makao makuu ya Tume leo
(jumatano Feb. 13, 2013) kuwasilisha mapendekezo yao juu ya muundo wa mabaraza
ya Katiba kwa jamii ya watu wenye ulemavu. Wa pili kushoto ni Mjumbe wa Tume,
Dkt. Salim Ahmed Salim.
Mkalimani wa lugha za
alama kwa watu wenye ulemavu wa kusikia kutoka Umoja wa Miradi ya Viziwi
Tanzania (UMVITA), Bi. Ruth Hope akisaidia uelewa wa lugha ya mawasiliano kwa
watu wa jamii ya walemavu wa kusikia katika mkutano baina yao na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba. Walemavu hao waliunda kamati iliyokutana na Tume ili
kuwasilisha mapendekezo yao juu ya muundo wa mabaraza ya Katiba kwa jamii
yao
Post a Comment