KLABU
ya soka ya Simba inasikitika kutangaza kifo cha mjumbe wake wa Kamati ya
Mashindano na Maendeleo ya Timu za Vijana, Hamis Mrisho maarufu kwa jila la
Hamis Dalali aliyefariki dunia alfajiri ya leo kijijini kwake Matimbwa, Bagamoyo
mkoa wa Pwani.
Mwenyekiti
wa Simba, Alhaji Ismail Aden Rage, amesema msiba huo ni mzito sana kwa klabu na
kwamba katika mechi ya kesho ya Ligi Kuu ya Vodacom, wachezaji na viongozi wa
Simba watavaa vitambaa vyeusi kuashiria msiba huo mzito.
"Kwa
niaba ya klabu ya soka ya Simba na kwa niaba yangu binafsi, naomba kutoa salamu
zangu za rambirambi za dhati kabisa kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa
marehemu kutokana na kifo cha ghafla ndugu Mrisho. Nilimfahamu kama mchapakazi
wa kweli na mtu aliyeipenda Simba kwa moyo wake wote," alisema
Rage.
Mrisho
ambaye pia alikuwa Katibu wa Matawi ya Simba Wilaya ya Kinondoni, alikuwa ni mtu
aliyekuwa akijituma sana kufanya kazi zozote za klabu kwa kadri ya maelekezo ya
uongoz na hakuwa na makundi huku akipendwa na watu wote waliokuwa
wakimfahamu.
Marehemu
alizaliwa mwaka 1965 na ameacha mjane na watoto wanne. Mazishi yake yanatarajiwa
kufanyika leo jioni huko Matimbwa, Bagamoyo.
Mwenyezi
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, AMEN.
Imtolewa
na
Ezekiel
Kamwaga


Post a Comment