![]() |
| Tenga |
Na Boniface
Wambura
RAIS wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ameteua wajumbe
wawili kuingia kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF baada ya nafasi mbili kuwa wazi
kutokana na mmoja kuteuliwa kuongoza kamati nyingine ya TFF na mwingine kufariki
dunia.
Iddi
Mtiginjolla ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati ya Nidhamu hivi karibuni aliteuliwa
kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF baada ya Shirikisho
kufanya mabadiliko ya katiba yaliyotokana na maagizo ya Shirikisho la Kimataifa
la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA), wakati mjumbe mwingine wa Kamati ya Nidhamu,
Shaaban Semlangwa alifariki dunia katikati ya mwaka
uliopita.
Wajumbe
wapya walioteuliwa ni Jesse Mguto- alikuwa Hakimu Mkazi na kwa sasa ni
mwanasheria na Wakili wa Mahakama Kuu. Ana Digrii ya Sheria. Mwingine ni Yohane
Masala ambaye kwa sasa ni Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali (Principal State
Attorney). Ana Digrii ya Kwanza na ya Pili ya Sheria na Digrii ya Pili katika
masuala ya Amani na Haki (MA in Peace and Justice).
Rais Tenga
amesema ana imani na uwezo wa watu hao na kwamba watafanya kazi yao kwa uadilifu
ili Shirikisho liendelee kuboresha utawala bora.



Post a Comment