Kamishna
wa Huduma za Urekebishaji wa Jeshi la Magereza, Dionece Chamulesile akitoa
hotuba ya kuufunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Pili wa TPS Saccos
uliofanyika mjini Morogoro.
Baadhi
ya viongozi wapya waliochaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha
Akiba na Kukopa cha Jeshi la Magereza (TPS Saccos) wakiwa mbele ya wajumbe hao
(hawapo pichani). Kushoto ni Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo, Joel Bukuku
akizungumza na wajumbe hao. Uchaguzi huo umefanyika katika Hoteli ya Edema,
mjini Morogoro.
Baadhi ya wajumbe wa
mkutano huo wakifurahia kupata viongozi wapya watakaokiongoza chama
hicho.
Wajumbe wa Bodi ya TPS
Saccos waliomaliza muda wao wakiondoka meza kuu na kuupisha uongozi mpya. Kulia
ni aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dionece Chamulesile, wa katikati ni Dk
Juma Malewa na Stanford Ntirundura waliokuwa wajumbe wa bodi
hiyo
PICHA ZOTE
NA
KITENGO
CHA MAWASILIANO
YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
YA
NCHI
Post a Comment