Mshitakiwa wa kwanza katika
kesi ya kumtolea lugha ya matusi mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mwita
Waitara Mwakibe akitoka nje ya mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida baada ya
kesi yao kuahirishwa leo, Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 11 mwaka huu,baada
ya mashahidi wa upande wa mashitaka kuingia mitini.
Wakili wa washitakiwa
vigogo wa CHADEMA Onesmo Kyauke (katikati) akiwaeleza jambo wateja wake muda
mfupi baada kesi ya wateja wake kuahirishwa hadi Machi 11 mwaka huu.Vigogo hao
wanaoshitakiwa kwa kumtolea lugha ya matusi mbunge wa jimbo la Iramba magharibi,
Mwigullu Lameck Nchemba. Dk.Kitila Mkumbo (kushoto) na afisa sera na utafiti,
Mwita Waitara Mwakibe (kulia).(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel
Limu.
Mashahidi watano wa upande
wa mashitaka yanayowakabili vigogo wawili wa CHADEMA taifa, wameingia mitini na
kusababisha kesi kuahirishwa kusikilizwa hadi Machi 11 mwaka
huu.
Mashahidi hao walikuwa
watoe ushahidi dhidi ya washitakiwa Afisa Sera na Utafiti wa CHEDEMA Makao Makuu
Mwita Waitara Mwikwabe (37) na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam na
Mshauri wa CHADEMA Dk.Kitila Mkumbo.
Vigogo hao wanatuhumiwa
kutoa lugha ya matusi kwa mbunge wa jimbo la Iramba magharibi Mwigullu Lameck
Nchemba.
Mwendesha mashitaka
mwanasheria wa serikali Mary Mudulugu amedai mbele ya hakimu mfawidhi wa
mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida Rusth Massam, kuwa askari polisi ambaye
ni mpelelezi wa kesi hiyo yupo Dar-es-salaam kitendo kilichopelekea mawasiliano
baina yao,yakatike.
Amesema kutokana na
mpelelezi huyo kuwa jijini Dar-es-salaam, mawasiliano na mashahidi hao watano
ambao ni wa mwisho katika kesi hiyo,yamekuwa magumu na yamesababisha washindwe
kufika mahakamani.
Kabla ya kuahirishwa kwa
kesi hiyo,wakili wa washitakiwa Onesmo Kyauke, aliiomba mahakama hiyo kutaja
tarehe ya mwisho kwa upande wa mashitaka kuleta mashahidi wao na endapo
watashindwa kuwaleta, mahakama ifunge ushahidi kwa upande wa
mashitaka.
Post a Comment