Na
Bryceson Mathias, Mvomero Morogoro
HALI ikiwa si shwari ndani ya
Halmashauri ya Wilaya Mvomero Morogoro, Madiwani walitoka nje ya mkutano kususia
kikao, huku wakimtelekeza ukumbini Mkurungenzi Sarah Linuma, wakipinga kufaya
kazi naye kutokana na kubainika matumizi ya Mil.469,721,961/-bila
Uhalili.
Uchunguzi uliofanywa
20.2.2013 nje ya ukumbi wa Halmashauri katika Kikao cha Dharula kilichokuwa
kikae kujadili Ukaguzi wa ndani ukiwa na madokezo ya makabrasha, walipoingia na
kumkuta Mkurugenzi akiwa amekaa Meza Kuu, waliamua kutoka nje.kuonesha
kumkataa.
Madiwani hao wakitarajia kwa
barua yenye kumbukumbu MVDC/CPF.49/14 ya tarehe
10.2.2013 waliyomwandikia
Mkuu wa Mkoa Joel Bendera yenye kuhusu kukataa kufanya kazi na Mkurugenzi Linuma
imeeleweka na kwamba asingekuwepo kwenye kikao hicho walipomuona waliudhiwa na
kuamua kutoka nje ya ukumbi wakimteleza na kumsusa hapo hapo.
“Tulishangazwa na Mkuu wa
Mkoa Bendera, kuunda Tume ya Uchunguzi wa tuhuma za Ubadhirifu huo badala ya
kumchukulia hataua, huku akimuacha Mkurugenzi huyo anaendelea kuwa kazini wakati
Mtu akituhumiwa na kuundiwa Tume, hastahili kuwa kazini hadi ukweli uwe
wazi.
“Madudu haya ndiyo
yanayotumaliza CCM, na hii ni aibu kwa madiwani wake kwa sababu awali zilikuwa
tuhuma za malipo hewa ya Ujenzi Mil. 53/-, ubadhirifu wa Mil. 58/-, na sasa Mil.
469,721,961/-, ni aibu kwa Wilaya, Mkoa, Taifa na wananchi. alisema Diwani wao
aliyeombwa asitajwe.
Mbali na Taarifa za kwenye
Mabrasha, Madiwani tangu kikao cha Dharula cha 28.1.2013 walipinga hayo hali
iliyopelekea Watumishi wanne (4), Ester Majagi (Ofisa Mipango), John Kuyi
(Mhasibu Matumizi), Anastazia Shosho na Stevin Tibenda (Watunza
Fedha). kusimamishwa kazi.
Licha ya Madiwani kumshukia
DED Linuma wakidai pengine anahusika na ubadhirifu huo, pia walihoji iwapo kuna
ukweli uliozagaa kwamba Mwenyekiti wa Halmashauri Jonas VanZealand ambaye pia
Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, kwamba alinunuliwa Magurudumu ya Mil.
6,900,000/-, jambo alilokanusha vikali mbele ya madiwani, hajawahi kupokea hata
senti.
Aidha Habari toka ndani ya
Halmashauri zimedai kuwepo tuhuma ya Mil.10/- kuchukuliwa ili kufanyia sherehe
ya Harusi ya Kigogo mmoja, jambo ambalo linafanyiwa uchunguzi kubaini ukweli
wake. Mkuu wa Mkoa Bendera akisubiri taarifa ya Tume yake Madiwani wameipinga na
kutishia kuibua Mgorogoro mkubwa wakidai watapeleka mashitaka kwa walipa
kodi.
Post a Comment