Mfuko wa Pensheni kwa
Watumishi wa Umma (PSPF) umekamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 641
katika mikoa mitano ambazo zilianza kuuzwa tangu Novemba mwaka 2012. Mradi huo
unalenga kutatua tatizo la makazi kwa wanachama wake na jamii kwa
ujumla.
Mikoa iliyojengwa nyumba
hizo na idadi ya nyumba katika mabano ni Dar es salaam – Buyuni (491), Morogoro
– Lukobe (25), Shinyanga – Ibadakuli (50), Tabora – Usule (25) na Mkoa wa Mtwara
– Mang’amba (50).
Aidha kwa Mujibu wa
maelezo ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bwana Adam Mayingu amewaambia
wanandishi wa habari na viongozi mbalimbali waliotembelea eneo la mradi huo Mkoa
wa Dar es Salaam kuwa Shirika lake limejenga nyumba za aina nne ambazo ni za
nyumba viwili, Vyumba vitatu, Nyumba za vyumba vitatu kimoja ikiwa ni Master na
Nyumba ya vymba vine kimoja kikiwa ni Master.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam Mayingu (katikati)
akiwaonesha maofisa wa Jeshi la Polisi moja ya nyumba 491 zilizopo katika mradi
wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu ambazo zitkopeshwa kwa wanachgama wa mfuko
huo. Nyumba hizo zipo katika eneo la Kigezi Kata ya Majohe wilaya ya Ilala
jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam Mayingu (kushoto) akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa ziara hiyo ya kuakagua
makazi hayo. Kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Hery Mohamed Kessy
Nyumba hizo zipo katika eneo la Kigezi Kata ya Majohe wilaya ya Ilala jijini Dar
es Salaam.
©MICHUZI
JR
Post a Comment