Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Seneta, Stive King, wakati alipofika
katika Ofisi yake iliyopo katika jingo la Ofisi za Maseneta wa Marekani, akiwa
katika ziara yake ya siku nne katika jiji la Washngton Dc nchini Marekani, Feb
6, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya
Watanzania waishio Washngton Dc, Feb 6, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya
Watanzania waishio Washngton Dc, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Feb 6,
2013, katika Hoteli ya Omni Shoreham.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya
pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania, nchini Marekani katika jiji la
Washngton Dc, baada ya mazungumzo yao alipowasili jijini humo kuanza ziara yake
ya siku nne, iliyomalizika jana Feb 7, 2013. Wa kwanza (kushoto) ni Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (wa tano kutoka kushoto) ni Naibu Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, Mahadhi Juma
Maalim.
Post a Comment