Malinzi
Na Prince Akbar
KAMATI ya Rufaa ya
Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jana imemuengua Mwenyekiti wa
Chama cha Soka Kagera (KRFA), Jamal Malinzi kugombea Urais wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF).
Taarifa ya TFF jana, imesema kwamba mgombea pekee
aliyepitishwa katika nafasi ya Urais, inayoachwa wazi na Leodegar Tenga ni
Athumani Nyamlani.
Nyamlani amepeta kuelekea uchaguzi huo, utakaofanyika
Februari 24, mwaka huu kwa sababu pingamizi alilowekewa limetupiliwa
mbali.
Wengine walioenguliwa ni Michael Wambura aliyekuwa akiwania nafasi ya
Makamu wa Rais na Ahmed Yahya aliyekuwa akiwania nafasi ya Uenyekiti wa Bodi ya
Ligi.
Malinzi aaliwekewa pingamizi Agape Fue, ambaye awali alishindwa na
kuamua kukata rufaa.
Malinzi |
Na Prince Akbar
KAMATI ya Rufaa ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jana imemuengua Mwenyekiti wa Chama cha Soka Kagera (KRFA), Jamal Malinzi kugombea Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Taarifa ya TFF jana, imesema kwamba mgombea pekee aliyepitishwa katika nafasi ya Urais, inayoachwa wazi na Leodegar Tenga ni Athumani Nyamlani.
Nyamlani amepeta kuelekea uchaguzi huo, utakaofanyika Februari 24, mwaka huu kwa sababu pingamizi alilowekewa limetupiliwa mbali.
Wengine walioenguliwa ni Michael Wambura aliyekuwa akiwania nafasi ya Makamu wa Rais na Ahmed Yahya aliyekuwa akiwania nafasi ya Uenyekiti wa Bodi ya Ligi.
Malinzi aaliwekewa pingamizi Agape Fue, ambaye awali alishindwa na kuamua kukata rufaa.
Post a Comment