MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya
Taifa (NEC) ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametoboa siri kwamba
mumewe, Rais Jakaya Kikwete pamoja sura yake kujawa haiba ya ucheshi wa
mara kwa mara lakini kwa tabia ana hasira.
Amesema, Rais Kikwete hukasirika sana anapoona au
kusikia mtu au mtendaji katika Chama au serikali anafanya mambo ya hovyo
au ya kizembe hasa katika masuala ya kazi.
Mama
Salma Kikwete ametoboa siri hiyo, leo Februari 18, 2013, kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kikwetu Kata ya Mbanja akiwa
katika ziara ya kukagua, kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji
wa ilani ya Chama na kuwashukuru wana-CCM wa Lindi mjini kwa kumchagua
kuwa mjumbe wao wa NEC.
"Siyo kweli kwamba Rais Jakaya Kikwete si mkali,
japokuwa ana sura yenye haiba ya ucheshi wa mara kwa mara kwa kila mtu,
lakini ana hasira, tena sana pale mtendaji au mtu yeyote anapombaini
kwamba anafanya mambo ya hovyo hovyo au ya kizembe katika kazi za Chama au
serikali yake", alisema Mama Salma Kikwete.
Mama Kikwete akitoa ufafanuzi, baada ya
mshereheshaji mmoja kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya
Lindi mjini Muhsin Ismail, kusema kwamba Rais Jakaya Kikwete ni mpole wa
kupindukia na kuuliza umati wa wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo
kwamba je ni nani amewahi kumuona amenuna.
"Natoa ofa kama hapa kuna mtu aliyewahi kumuona
mpendwa wetu, Rais Kikwete amenuna anyooshe mkono. Akitokea ntampa sh.
elfu moja hapa hapa... Kwa mara ya kwanza, ya pili unaona hakuna",
alisema Muhsini.
Wakati akiendelea kusema hivyo, mtu mmoja kwenye
mkutano huo alinyoosha mkono, lakini Muhsin akakataa kumpa zawadi yake
kama alivyokuwa ameahidi. "Aaa wewe sikupi zawadi", alisema Muhsini
lakini papo hapo akakatishwa na Mama Mama Kikwete.
"Hata kama humpi hiyo zawadi, sawa. lakini Siyo
kweli kwamba Rais Jakaya Kikwete hakasiriki na siyo mkali. Japokuwa ana
sura yenye haiba ya ucheshi wa mara kwa mara kwa kila mtu, lakini ana
hasira, tena sana pale mtendaji au mtu yeyote anapombaini kwamba
anafanya mambo ya hovyo ay ya kizembe..." alisema Mama Kikwete.
NA BASHIR NKOROMO, LINDI
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCN, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametoboa siri kwamba
mumewe, Rais Jakaya Kikwete pamoja sura yake kujawa haiba ya ucheshi wa mara kwa mara lakini kwa tabia ana
hasira.
Amesema, Rais Kikwete hukasirika sana anapoona au kusikia mtu au mtendaji katika Chama au serikali anafanya
mambo ya hovyo au ya kizembe hasa katika masuala ya kazi.
Mama Salma Kikwete ametoboa siri hiyo, leo Februari 18, 2013, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji
cha Kikwetu Kata ya Mbanja akiwa katika ziara ya kukagua, kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa ilani
ya Chama na kuwashukuru wana-CCM wa Lindi mjini kwa kumchagua kuwa mjumbe wao wa NEC.
"Siyo
kweli kwamba Rais Jakaya Kikwete siyo mkali, japokuwa ana sura yenye
haiba ya ucheshi wa mara kwa mara kwa kila mtu, lakini ni ana hasira,
tena sana pale mtendaji au mtu yeyote anapombaini kwamba anafanya mambo
ya hovyo ay ya kizembe katika kazi za Chama au serikali yake", alisema
Mama Salma Kikwete.
Mama Kikwete akitoa ufafanuzi, baada ya
mshereheshaji mmoja kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya
Lindi mjini Muhsin Ismail, kusema kwamba Rais Jakaya Kikwete ni mpole wa
kupindukia na kuuliza umati wa wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo
kwamba je ni nani amewahi kumuona amenuna.
"Natoa ofa kama hapa kuna mtu aliyewahi kumuona
mpendwa wetu, Rais Kikwete amenuna anyooshe mkono. Akitokea ntampa sh.
elfu moja hapa hapa... Kwa mara ya akwanza, ya pili unaona hakuna",
alisema Muhsini.
Wakati akiendelea kusema hivyo, mtu mmoja kwenye
mkutano huo alinyoosha mkono, lakini Muhsin akakataa kumpa zawadi yake
kama alivyokuwa ameahidi. "Aaa wewe sikupi zawadi", alisema Muhsini
lakini papo hapo akakatishwa na Mama Mama Kikwete.
"Hata kama humpi hiyo zawadi, sawa. lakini Siyo
kweli kwamba Rais Jakaya Kikwete hakasiriki na siyo mkali. Japokuwa ana
sura yenye haiba ya ucheshi wa mara kwa mara kwa kila mtu, lakini ni ana
hasira, tena sana pale mtendaji au mtu yeyote anapombaini kwamba
anafanya mambo ya hovyo ay ya kizembe..." alisema Mama Kikwete
Post a Comment