PAMBANO la Ligi ya
Mabingwa Afrika kati ya Simba na Libolo FC ya Angola lililofanyika jana (Februari 17 mwaka
huu) limeingiza sh. 133,795,000 wakati lile la Kombe la Shirikisho kati ya Azam
na El Nasir ya Sudan Kusini lililochezwa juzi (Februari 16 mwaka huu) limeingiza
sh. 34,046,000.
Watazamaji 22,469
walikata tiketi kushuhudia mechi ya Simba kwa viingilio vya sh. 5,000, sh.
10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Simba ilipoteza pambano hilo kwa bao 1-0.
Mgawo wa mechi hiyo
ulikuwa kama ifuatavyo; gharama za waamuzi sh. 24,926,500, gharama za tiketi sh.
7,410,000, asilimia 15 ya uwanja baada ya kuondoa gharama za waamuzi na tiketi
ilikuwa sh. 15,218,775, asilimia 10 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 10,145,850 na asilimia 75
iliyokwenda klabu ya Simba ni sh. 76,093,875.
Mechi ya Azam
iliyomalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 ilishuhudiwa na
watazamaji 13,431 kwa viingilio vya sh. 2,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh.
20,000. Mgawo katika mechi hiyo ulikuwa kama ifuatavyo;
Gharama za tiketi sh.
4,779,000, asilimia 15 ya uwanja baada ya kuondoa gharama za tiketi ilikuwa sh.
4,390,050, asilimia 10 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 2,926,700 na asilimia 75
iliyokwenda Prime Time Promotions (Azam) ni sh.
29,267,00.
Post a Comment