
Aidha CUF imewatangazia
neema Watanzania kuwa endapo itachukua madaraka katika uchaguzi huo itawajaza
fedha mifukoni ikiwa ni njia mojawapo ya kuwaondolea umasikini.
Makamu huyo wa kwanza wa
rais alisema hayo katika mkutano wa uzinduzi wa oparesheni ya mkachamchaka
kuelekea mwaka 2015 (V4C), uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi
Kiwanja cha Ndege, manispaa ya Morogoro.
Alisema Profesa Lipumba
bado ni kiongozi shupavu anayestahili kugombea wadhifa huo kupitia CUF katika
uchaguzi ujao kwakuwa anakubalika ndani ya chama hicho pamoja na kwa
wananchi.
Post a Comment