Waziri wa Uchukuzi Mhe.
Dkt. H. Mwakyemba, (Aliyesimama) akiongea mbele ya Rais wa kwanza wa Zambia
Mhe. Kenneth Kaunda wakati wajumbe kutoka Tanzania walipomtembelea Rais huyo
katika ofisi zake. Wengine katika picha ni wajumbe wa Bodi ya Tazara kutoka Tanzania.
Rais wa Kwanza wa Zambia
Keneth Kaunda wa nne kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa
Tanzania na Zambia. Kulia kwa Mhe. Kaunda ni Balozi wa Tanzania nchini Zambia
mama Grace Mujuma na anayefuata ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Eng. Omar
Chambo. Kushoto kwa Mhe. Kaunda ni Waziri wa Uchukuzi Mhe. Dkt. Mwakyembe,
akifuatiwa na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum na anayefuta ni Waziri wa
Uchukuzi wa Zambia Mhe. Christopher Yaluma, Wengine katika picha ni Wajumbe wa
Bodi ya TAZARA kutoka Tanzania.
***********
Waziri wa Uchukuzi, Mhe.
Dkt. Harrison Mwakyembe katikati ya wiki hii aliongoza ujumbe wa Tanzania
nchini Zambia katika kikao cha 58 cha Baraza la Mawaziri wanaosimamia
uendeshaji wa Reli ya Tazara. Kikao hiki cha siku mbili kiliwajumuisha Mhe.
Dkt. Harrison Mwakyembe (Uchukuzi), Mhe. Saada Salum (Fedha) na Mhe. Dkt.
Abdallah Kigoda (Viwanda na Biashara) na Mawaziri wa sekta husika kutoka
Zambia. Aidha, kikao hiki kilitanguliwa na kikao cha Bodi ya TAZARA. Ujumbe wa
Tanzania ukiwa nchini humo uliweza kumtembelea Rais wa kwanza wa Zambia Mhe.
Kenneth Kaunda katika ofisi zake ambapo katika kikao cha pamoja na Rais huyo,
Mhe. Kaunda alisisitiza mshikamano na upendo miongoni mwa waafrika na
kuwahimiza ‘vijana’ viongozi waliopewa jukumu la kusimamia TAZARA kufanya kazi
kwa bidii ili kuongeza ufanisi wa RELI hii ili iendelea kuwasaidia wananchi wa
nchi zote mbili.
credits: Michuzi Blog
Post a Comment