Wameuawa
kisha kuchinjwa na kuchomwa moto ndivyo miili ya marehemu wanaodhaniwa
kuwa ni majangiri wa wanyama poli inavyoonekana ilipofikishwa
kuhifadhiwa katika hospital ya Mvumi Dodoma.
Mwili
wa Mtu anayedhani wa kuwa ni Jangili ukiwa umehalibika baada ya kuuawa
kuchinjwa na kuchomwa moto katika chumba cha kuhifadhia maiti mvumi
Dodoma.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Dodoma David Misime akiwaonyesha waandishi wa Habari
meno 73 ya tembo yenye thamani ya zaidi 225 mil ambayo ni sawa na tembo
36 pamoja na Gari aina ya Noah NO T 983 BZJ waliokamata juzi katika
kijiji cha Miganga mvimi wilayani Chamwino Dodoma.
Kamanda
wa polisi Mkoa wa Dodoma David Misime akifafanua jambo mbele ya
waandishi wa Habri kuhusu tukio la vifo vya watu watatu wanaodhaniwa
kuwa ni majangili waliouawa na wananchi katika kiji cha miganga Mvumi
Dodoma pembeni ni Gari aina ya Noah No T 983 BZJ walilokuwa wakilitumia
na kuku meno 73 ya Tembo.
Na John
Banda, Dodoma
MAJANGILI
watatu wa nyara za serekali wameuawa kwa mishale yenye sumu na kisha miili yao
kuchomwa moto na wananchi katika purukushani na polisi walipokuwa wakijaribu
kukimbia ili kutorosha meno ya tembo.
Tukio hilo
lilitokea jioni ya alhamis wiki hii katika kijiji cha Miganga kata ya mvumi
wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma ambapo miili yao ilikutwa ikiwa imehalibika
kutokana na kuchomwa moto.
Akizungumzia
tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma David Misime alisema majangili hayo
yaliuawa na wanachi wenye hasira kali kwa zana mbalimbali za kijadi walipokuwa
wanakimbilia polini ili kujiokoa na mkono wa polisi.
Misime
alisema jeshi hilo lipokea taarifa kutoka kwa wananchi wema kuwa kulikuwa na
Gali likitokea Manda likiwa na Meno ya Tembo na kisha kuweka mtego katika kijiji cha
mwitikila ambapo waliona gali aina ya NOAH T 983 BZJ na kulisimamisha na Dereva
wa Gali hilo alifanya kama anapunguza mwendo na kisha kuondoka kwa mwendo wa
kasi.
‘’Polisi
wakishirikiana na wananchi walianza kulifukuza walipofika kijiji cha Miganga Mvumi polisi
walifanikiwa kupiga Risasi tairi moja ya kushoto na hivyo watu watatu
waliokuwemo ndani gari hilo waliruka na kutawanyika, wananchi waliojichukulia
sheria mkononi waliwashambulia kuasi cha kupoteza maisha yao’’, alisema
Aidha kamanda
Misime alisema baada ya kulipekua Gari hilo walikutaMeno 73 ya Tembo yenye
uzito wa kilo 255.9 yakiwa na thamani ya zaidi ya TSH 225 mil pamoja na hati ya
mashitaka [CHARGE SHEET] ambayo ni kesi ya kuhujumu uchumi namba 4/2012
iliyokuwa imefunguliwa katika mahama yam panda mkoa wa katavi na Leseni ya
Udereva na 4000692535 Aboubakar Peter huku wakihisi ni mmoja ya waliouawa.
Alisema
walikuwa wameshitakiwa kwa kosa la kupatikana na Meno 3 ya Tembo Tarehe
17.06.2012 na maafisa wanyama poli
katika eneo la Msaginya Wilaya ya Mlele mkoa wa katavi majina ya
walikuwa wameshatakiwa ni Joseph Marius [NGONDO] 59 mkazi wa maili mbili
Dodoma, Aboubakar Mhina 25 mkazi wa Mkuhungu Dodoma, Msafiri Milawa 36 mkazi wa
Nkuhungu Dodoma na Petro Mtipula 55 mkazi wa mpanda.
Kamanda
alitoa wito kwa wananchi wasijichukulie Sheria mikononi kwani kwa kufanya hivyo
ni kupoteza ushahidi na inawawia vigumu polisi kupata mtandao inayohusika na
matukio kama hayo.PICHA NA JOHN BANDA WA PAMOJAPURE BLOG
Post a Comment