|
Meli
ya kivita ya kupambana na uharamia aina ya Anti Submarine iitwayo
Marshal Shaposhnikov’, ilipokuwa ikiingia na kasha baadae kutia nanga
katika bandari ya Dar es Salaam, kwa ziara fupi yenye lengo la
kuimarisha urafiki baina ya Jeshi la Wanamaji wa Tanzania na Urusi. Wakati
nchi ya Somalia ikiendelea kuwa kitovu cha uharamia, jumuiya ya
kimataifa ilikubaliana kudhamiria kupambana na vitendo hivyo viovu.
Lakini hadi sasa, wakati nchi nyingine zikitumia mbinu mbalimbali katika
mapambano hayo, ni nchi za Russia, India na China pekee zinazosindikiza
meli zao za biashara na nyinginezo ili kuzilinda na uharamia. Meli hiyo
imewasilisiku ya Jumamosi na inategemea kuondoka kesho, Jumatano.
|
|
Balozi wa Urusi hapa nchini Mheshimiwa Alexander Rannikh akiambatana na kiongozi wa wanajeshi waliofatana na meli hiyo Rear Admiral Vdovenko |
|
Kwa pamoja, Balozi Rannikh na wanajeshi wa Kirusi waliimba wimbo wao wataifa wakiwa katika meli.
|
|
Balozi Rannikh akiwapongeza wanajeshi wake kwa kufika Dar es Salaam, Tanzania na kuwakaribisha nchini pia. |
|
Baada ya salamu hizo, Balozi Rannikh nae alikaribishwa keki na mmvinyo iliyoandaliwa na wanajeshi katika meli. |
|
Balozi
wa Urusi hapa nchini Mheshimiwa Alexander Rannikh akipokea salamu
kutoka kwa kiongozi mkuu Rear Admiral Vladimir Vdovenko wakati
alipotembelea meli hiyo bandarini. |
Wanajeshi wa Kirusi wakionesha umahili wao wa ukakamavu
on Tuesday, February 19, 2013
Post a Comment