JESHI la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia
watu watatu wa familia mmoja wakazi wa eneo la Ruvuma chini lililopo katika
Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa tuhuma za kukutwa na kiganja cha binadam
ambacho kimekutwa ndani ya duka la
linalomilikiwa na familia hao.
Habari zilizopatikana
jana ambazo zimezibitishwa na kaimu kamanda wa mkoa wa Ruvuma George Chiposi
zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea February16 mwaka huu saa za mchana huko
katika eneo la Ruvuma chini nje kidogo na Manispaa ya
Songea.
Kaimu kamanda wa polisi
Chiposi amewataja wanaoshikiriwa kuwa ni Denis Kalsinje (42) ambaye ni mfanya
biashara na ni mkazi wa eneo la Ruvuma chini, Sabina Hakika (38) maarufu kwa
jina la Mduma ambaye ni mke waDenis Kalsinje na Emmanuel Kalsinje (36) ambaye ni
mdogo wa Denis Kalsinje.
Chiposi alimwambia
mwandishi wetu jana mchana ofisini kwake kuwa polisi ilipata taarifa kutoka kwa
raia wema kuwa kunamfanyabiashara mmoja huko katika eneo la Ruvuma chini
anafanya biashara sana kwa vile ameweka kiganja cha binadam kwenye duka lake
ambacho inadaiwa kuwa ndicho kinachokuwa kinavuta wateja taarifa ambayo polisi
ilifanyia kazi kikamilifu.
Alisema kuwa February 16
mwaka huu majira ya saa tano asubuhi mkaguzi msaidizi wa polisi Karimu Mtikula
akiwa na askari polisi wenzake waliondoka wakitokea ofisi ya Mkuu wa upelelezi
ya makosaya jinai mkoa wa Ruvuma walienda hadi kwenye eneo la Ruvuma chini
ambako walifika kwenye eneo la tukio na kufanya upekuzi wa kina ndani ya duka la
mfanya biashara huyo Denis na kufanikiwa kukipata kiganja kimoja cha mkono wa
kushoto wa binadam.
Alifafanua zaidi kuwa
inadaiwa kiganja hicho kilikutwa kimehifadhiwa kwenye kasha la kuhifadhia
marashi ambalo liliandikwa Blue For man na kuviringishwa kwenye mifuko mitatu ya
Rambolikiwa ndani ya duka la mfanya biashara huyo.
Hatahivyo Kaimu kamanda
Chiposi alisema kuwa katika mahojiano ya awali mfanyabiashara huyo Kalsinje
alikili kukutwa na kiganja cha binadam kwenye duka lake lakini anashindwa
kuelewa ni nani aliye kileta na kukiweka ndani ya duka
lake.
Alieleza kuwa katika
tukio hilo watuhumiwa hao wamesha kamatwa na kwamba kwa sasa hivi polisi
inaendelea kufanya upelelezi zaidi wa tuki hilo na ukikamilika watuhumiwa
watapelekwa mahakamani kujibu mashitaka yao yanayo
wakabili

Post a Comment