Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Injinia Stella Manyanya akizungumza katika kikao cha baraza la ushauri la
watumiaji wa nishati na maji nchini na wadau wake walipotembelea Mkoani Rukwa
kwa ajili ya shughuli mbalimbali za baraza hilo. Mkuu huyo wa Mkoa alitoa
pongezi kwa kazi nzuri wanayofanya na kuahidi kuwachukulia hatua walanguzi wa
nishati ya mafuta pamoja na wale wanasimamia kwa kushindwa kufanya kazi yao
vizuri. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed
Chima.
Mwenyekiti
wa baraza la ushauri watumiaji wa maji na nishati nchini Eng. Profesa Katima
akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema kazi kubwa ya baraza hilo ni
kutetea na kulinda haki za watumiaji wa maji na nishati ambayo ni maji safi na
maji taka, umeme, petroli na gesi asilia.
Baadhi
ya wadau wa mkutano huo ambao ni vyombo vya ulinzi na usalama, Tanesco, EWURA
Mkoa wa Rukwa, wawakilishi wa sheli za mafuta na shirika la Maji safi na Maji
taka Mkoa wa Rukwa (SUWASA)
Wawakilishi wa baraza hilo
Mkoani Rukwa
Picha ya
pamoja.
(Na Hamza Temba -Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa Rukwa –
rukwareview.blogspot.com)
Post a Comment