Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Montage,Teddy Mapunda (katikati) akizungumza na Waandishi wa habari
(hawapo pichani) wakati akitandaza kufanyika kwa tafrija maalum ya harambee ya
kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya afya hapa
nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball,itakayofanyika Februari 22 kwenye
Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam.ambapo malengo ni kukusanya kiasi cha
zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Wanawake wenye
matatizo mbali mbali.Mgeni rasmi katika Tafrija hiyo anatarajiwa kuwa Mwenyekiti
wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA),Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.Kulia
ni Meneja Masoko na Mauzo wa Serena Hoteli,Seraphin Lusala na kushoto ni
Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi ya Tafrija hiyo,Barbara Hassan.
Meneja Masoko na Mauzo wa
Serena Hoteli,Seraphin Lusala akifafanua jambo kwa wanahabari juu ya tafrija
hiyo.
Mwenyekiti Kamati ya
Maandalizi ya Tafrija hiyo,Barbara Hassan akizungumzia maandalizi
yalivyofikia.Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Montage,Zainab
Mkindi.
on Monday, February 18, 2013
Post a Comment