Mwenyekiti
wa chama cha watu wenye ulemavu Tanzania (TAS) “Tanzania Albino Society” ndugu
Ernest Kimaya akizungumza kwa uchungu mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia
Stella Manyanya (Pichani chini) kuelezea juu ya tukio la kinyama alilofanyiwa
Maria Chambanenge (39) la kukatwa mkono wake wa kushoto kwa kile kinachodaiwa
kwa imani za kishirikina kuwa ni kupata utajiri. Watuhumiwa waliohusika na tukio
hilo ambao pia yupo mume wake na muathirika wameshakamatwa na polisi na
kuonyesha mkono huo, taratibu za mashitaka zinaendelea ili haki iweze
kupatikana. Mwenyekiti huyo ameiomba Serikali kufkiria adhabu kali kwa
watuhumiwa kama ho ikiwepo kunyongwa ili fundisho kwa wengine na Albino waweze
kuishi katika nchi yao kwa amani.
Mwenyekiti wa TAS
akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ofisini kwake. Kulia ni Katibu Mkuu wa
chama hicho ndugu Mohammed Chanzi.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kwa uchungu na kutoa onyo
kali kuwa vitendo hivyo vya kinyama havitavumiliwa. Alitoa wito kwa wananchi
kuendelea kutoa ushirikiano kutokomeza vitendo
hivyo.
Kabla
ya kwenda kumtembelea mgongwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliandaa chakula kwa wageni
wake.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na msafara wake pamoja na viongozi wa
chama cha Albino Tanzania (TAS) wakimfariji Mama Maria Chambanenge
walipomtembelea katika hospitali kuu ya Mkoa Rukwa ambapo hali yake kwa sasa
inaendelea vizuri japo ameongezewa ulemavu mwingine wa viungo kwa kukatwa mkono
wake wa kushoto.
Mwenyekiti
wa chama cha watu wenye ulemavu Tanzania (Albino) ndugu Ernest Kimaya akimfariji
Mama Maria Chambanenge ambaye anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali kuu
ya Mkoa Rukwa kufuatia kukatwa mkono wake wa kushoto na watu walioshirikiana na
mume wake na ambao tayari wapo mikononi mwa
polisi.
Post a Comment