Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Malimi Malemi (wa pili kutoka kushoto) akiangalia nyuzi za mkonge ambazo
zimeanikwa kwa ajili ya kukaushwa maji kabla ya kuingizwa kiwandani kwa ajili ya
kuzilainisha na kuzisafisha. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna
Jenerali John Minja.
Msimamizi wa Kiwanda cha Kuzalisha Nyuzi za Mkonge cha
Gereza Kihonda lililopo mkoani Morogoro, Fidelis Muhaya akimuonyesha majani ya
mkonge ambayo yamevunwa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Malimi Malemi (Kushoto). Katikati ni Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya
Sekta ya Sheria nchini, Wanyenda Kutta.
Naibu Katibu Mkuu,
Mwamini Malemi (katikati) akizishika nyuzi za mkonge zilizokamilika
ambazo zipo tayari kwa ajili ya matumizi mbalimbali nchini.
Naibu Katibu Mkuu,
Mwamini Malemi (katikati) na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna
Jenerali John Minja (kushoto) pamoja na wageni wengine wakionyeshwa pamoja na
kufafanuliwa zaidi na Msimamizi wa kiwanda hicho Fidelis Muhaya jinsi
inavyofanya kazi mashine ya kubana mkonge kwa ajili ya kupunguzwa
ukubwa.
Naibu Katibu Mkuu, Mwamini Malemi (wa pili kutoka
kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja
(kulia) pamoja na wageni waliotembelea kiwanda hicho wakiangalia mashine ya
kubana mkonge kwa ajili ya kupunguza ukubwa kabla ya
kusafirishwa.
PICHA ZOTE
NA
KITENGO CHA MAWASILIANO YA
SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA
NCHI.
Post a Comment