Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi
akimsalimia Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Sekta ya Sheria
nchini, Wanyenda Kutta (Kulia) wakati alipokuwa anawasili katika Ukumbi
wa Mikutano wa Edema mjini Morogoro kwa ajili ya kufunga rasmi mafunzo
ya Jinsia kwa maafisa mbalimbali wa Jeshi la Magereza. Kushoto ni
Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi
akizungumza na maafisa mbalimbali wa Jeshi la Magereza kabla ya kufunga
mafunzo ya jinsia kwa maafisa hao. Malemi licha ya kulipongeza jeshi
hilo kwa hatua nzuri ya kuwateua maafisa mbalimbali wanawake, alilitaka
jeshi hilo kuongeza juhudi zaidi kwa kuwapa nafasi ya uongozi wanawake
ambao wana uwezo na sifa ya kuongoza.
Maafisa Magereza wakiifurahia hotuba ya mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi alipokuwa anatoa hotuba ya kufunga mafunzo ya jinsia yaliyokuwa yanafanyika mjini Morogoro.
Naibu
Katibu Mkuu Mwamini Malemi (wa pili kutoka kulia) akimpa zawadi askari
wa Jeshi la Magereza kutoka Gereza la Wilaya ya Liwale, mkoani Lindi,
Beatrice Sabo kwa kuwasilisha vizuri mada ya jinsi na jinsia wakati wa
mafunzo hayo. Wa kwanza kutoka kushoto ni Kamishna wa Sheria na Utawala
wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa. Anayefuata ni Mshauri wa Masuala
ya Jinsia wa Programu ya Mabadiliko ya Sekta ya Sheria nchini, Bi.
Wanyenda Kutta. Kulia ni Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Chuo Kikuu
Cha Dar es Salaam, Asina Omari.
Naibu
Katibu Mkuu Mwamini Malemi (Kulia), akipokea taarifa ya hali ya
Utekelezaji wa Masuala ya Jinsia katika Taasisi zinazotekeleza Programu
ya Maboresho ya Sekta ya Sheria kutoka kwa Mshauri wa Masuala ya Jinsia
wa Programu ya Mabadiliko ya Sekta ya Sheria nchini, Bi. Wanyenda Kutta .
Kushoto ni Dk Juma Malewa, Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la
Magereza. PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI. WIZARA YA
MAMBO YA NDANI YA NCH
Post a Comment