Chama
cha NCCR – Mageuzi kimesema kimesema kimepokea kwa masikitiko makubwa
taarifa ya Katibu wa Bunge kwa waandishi wa habari juu ya mpango wa
kuzuia kurusha matangazo moja kwa moja na badala yake kuyafanyia kwanza
uhariri kabla ya kuwafikia walaji.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu wa chama
hicho Faustin Sungura NCCR – Mageuzi inapinga kwa nguvu zote, hatua
zozote zinazotaka kuchukuliwa na mamlaka yeyote za kuzuia matangazo ya
moja kwa moja kutoka bungeni.
Amesema
wanapinga hatua hizo kwa sababu, hoja na sababu za kutekeleza azma hiyo
kama zilivyotolewa na Katibu wa Bunge ni hoja dhaifu na hasi.
Amesema mawazo ya Katibu wa bunge yanakinzana na Ibara ya 18(d) ya katiba ya nchi
Post a Comment