Ndugu zangu,
Katika kitabu chake; The Flags Changed At Midnight- Mwandishi na ambaye alikuwa DC wa Mkoloni kuanzia 1951-62, Bw. Michael Longford anaelezea jinsi Serikali ya Mwingereza ilivyokuwa makini.
Anasema, kuwa aliyethubutu kuchezea shilingi ya Serikali alijuta kuzaliwa
.
Naam, kila siku inayoyoma. vichwa vya habari vya magazeti vina habari za kustusha. Kuna mahali tutaambiwa kuna ' Moto umewaka', na kwingine tutaambiwa ' kuna mamilioni yametafunwa!'
Na kesho kutwa itaingia kama vile hakuna kilichotokea jana yake.
Ndio, nchi yetu iko kwenye hali ya mkanganyiko- Delirium. Nimelisema hilo juzi.
Na ng'ombe wa Serikali huzikwa na ngozi yake. Ni nani anayejali? Maana, kama ng'ombe ni wa mtu binafsi, basi, akifa, atahakikisha walau anachuna ngozi yake, ili walau aambulie senti kidogo!
Na hilo ni Neno la Leo
Maggid Mjengwa,
Iringa
0788 111 765

Post a Comment