Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Dkt Fenella Mukangara
WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk
Fenella Mukangara anatarajiwa kufungua mbio za 11 za Kilimanjaro Marathon
zitakazofanyika Jumapili hii mjini Moshi.
Mkurugenzi Mkuu wa Executive Solutions ambao ndiyo
waratibu wa mbio hizo, Aggrey Marealle alithibitisha uwepo wa Waziri Mukangara
siku hiyo na kueleza kuwa ndiye atazifungua mbio hizo sambamba na kutoa zawadi
kwa washindi.
Tayari washiriki zaidi ya 6,000 kutoka nchi zaidi ya 40
wamethibitisha kushiriki kwenye mbio hizo zitakazofanyika katika makundi ya mbio
ndefu za marathon (km 42), nusu marathoni (km21) na mbio za km 5 za
kujifurahisha.
"Waziri Mukangara atashiriki pia katika hafla ya utoaji
zawadi kwa washindi 10 bora wa mbio za km 42 (Kilimanjaro Premium Lager
Marathon) kwa wanaume na wanawake,"alisema Marealle.
Kwa mujibu wa Marealle, mbali na Waziri Mukangara,
viongozi mbalimbali wa Serikali akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas
Gama watashiriki kwenye mbio hizo.
"Mbio za Kilimanjaro Marathon zinaiweka Tanzania kwenye
ramani ya kimataifa kila mwaka, pia zinatoa fursa kwa wanariadha wa ndani kukua
zaidi, kukuza utalii wa Tanzania na watu kupata nafasi ya kujenga afya zao,"
alisema Marealle.
Marealle
alibainisha kuwa mbio hizo zitakuwa na hadhi ya kimataifa ambapo zitasimamiwa na
klabu ya Kilimanjaro Marathon, Chama cha Riadha Tanzania (AT) na kile cha Mkoa
wa Kilimanjaro.
"Ilikuhakikisha
usalama wa wakimbiaji, baadhi ya barabara za ndani na nje ya mji wa Moshi
zitafungwa kuanzia saa 12:15 asubuhi hadi 03:30 asubuhi siku hiyo kwa lengo la
kuwapa fursa wakimbiaji kupita salama,"alisema Marealle.
Mbio hizo
zinadhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chao cha
Kilimanjaro Premium Lager, Vodacom Tanzania (iliyodhamini mbio za Km 5 Fun Run),
GAPCO (Nusu Marathon kwa Walemavu), Tanga Cement, CFAO Motors, KK Security, Keys
Hotel, TPC Sugar, Tanzanite One, New Arusha Hotel, UNFPA, Fastjet na Kilimanjaro
Water
Post a Comment