Na: GLADNESS MUSHI - ARUSHA
MFUKO wa taifa wa hifadhi ya Jamii (NSSF)unatarajia kuwekeza katika zao la Korosho ambapo watajenga kiwanda Mjini Mtwara kitakachogarimu kati ya Dola za Kimarekani milioni 35 na 45 hivi karibuni huku lengo halisi likiwa ni kuongeza uchumi wa Mikoa ya Lindi na Mtwara
Hayo yameelezwa na Dkt Ramadhani Dau ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa NSSF mapema leo wakati akizungumza na wadau wa mfuko huo katika mkutano wa tatu unaoendelea mjini hapa. Dkt Dau alisema kuwa kwa sasa NSSF wamefikiria jinsi ya kusaidia mikoa hiyo miwili ambayo ina kilimo kizuro cha Korosho lakini bado wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa kiwanda hivyo kama wataweza kujenga kiwanda hicho watawasaidia sana wakulima
Alisema kuwa mpango huo utakamilika mara baada watakapoongea na Uongozi wa Wilaya ya Tandahimba kwa ajili ya kuwekeana mikataba mbalimbali hivi karinbuni ili
Alisema kuwa mpango huo utakamilika mara baada watakapoongea na Uongozi wa Wilaya ya Tandahimba kwa ajili ya kuwekeana mikataba mbalimbali hivi karinbuni ili
waaanze rasmi uwekezaji wa zao hilo la Korosho ambalo linasoko kubwa sana ndani ya Tanzania na hata nje ya Tanzania.
‘kwa sasa wakulima wa zao la Korosho wanapata shida sana kutokana na
hali iliopo lakini kama tutaweza kuwekeza zaidi kwenye zao hilo ni
wazi kuwa thamani ya zao hilo itaweza kuongezeka sana,hivyo tunaitaji
kwa kweli ushirikiano baina ya wadau mbalimbali pamoja na uongozi wa
Wilaya husika ili lengo letu liweze kutimia tena kwa wakati”aliongeza
Dkt Dau.
Katika hatua nyingine Dkt Dau alisema kuwa uwekezaji huo utakuwa na
faida kubwa sana kwa kuwa wakulima wa zao la Korosho ndani ya mikoa
ya Lindi na Mtwara wanalazimika kuuza korosho zao kwa kiasi cha Dola
Moja baada ya Korosho kubaguliwa hali ambayo inazaa hasara kubwa sana
wakati mara baada ya kumalizika kwa uwekezaji huo wa Korosho wakulima
watalazimika kuuza Korosho zao kwa kiasi cha Dola saba baada ya
kubaguliwa,hivyo wakulima wa zao hilo watanufaika sana na uwekezaji
huo.
Mbali na hayo alisema uwekezaji huo utaweza kuongeza na kuimarisha
zaidi uchumi wa mikoa ya Lindi na Mtwara, lakini pia utachanngia kwa
kiwango kikubwa sana kuweza kuongezeka kwa ajira kwani asilimia kubwa
sana ya wakulima ambao wanalima zao hilo bado hawana ajira za kutosha
kutoka na uwekezaji hafifu ndani ya zao hilo hasa kwa mikoa hiyo.
Katika hatua nyingine wadau wa mkutano huo walisema kuwa ni vema kama
NSSF ikahaikisha kuwa inajiwekea utaratibu wa kuwekeza zaidi katika
Viwanda hususani viwanda ambavyo vimekufa kwani viwanda vinanafasi
kubwa sana ya kuibua Ajira hivyo Taifa litaweza kuondokana na
Umaskini.
Wadau hao walisema kuwa kwa sasa ndani ya nchi ya Tanzania kuna
viwanda vingi sana ambavyo vimekufa kutokana na uwekezaji huku viwanda
hivyo vikitumika kama magodaoni ya watu ingawaje Jamii bado
inakabiliwa na uhaba wa ajira,hivyo mfuko huo unatakiwa kuhakikisha
kuwa unaendelea kubuni aina mpya y a uwekezaji wa viwanda ambavyo
vilikuwepo lakini vikafa kwa maslahi ya Taifa.
“Mifuko ya Kijamii ina nafasi kubwa sana ya kufufua Viwanda kwa mfano
kwa zao la Korosho kiwanda kilikuwepo Pwani lakini kikafa na wakulima
wanapata shida na zao hilo linakosa Ubora unaotakiwa sasa mifuko hii
kama itaendelea kubuni aina mpya ya uwekezaji wa zao hilo basi
itachangia kwa kiwango kikubwa sana kuwasaidia wakulima ambao kwa sasa
robo tatu yao wanalima kwa ,mazoea tu hawalimi kwa ajili ya
kuthaminisha zao”waliongeza Wadau hao
Post a Comment