Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Jakaya Mrisho Kikwete leo anatarajiwa kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa maofisa wakuu waandamizi wa Polisi mjini Dodoma, utakaowashirikisha makamanda wote wa mikoa na vikosi utakaodumu kwa siku nne.
Akizungumza na Waandishi wa
Habari jana Mjini Dodoma, Msemaji wa Jeshi hilo Bi. Advera Senso alisema Lengo
la mkutano huo ni kujadili mambo mbalimbali ya kiutendaji ikiwemo utekelezaji wa
maazimio yaliyoafikiwa katika mkutano wa mwaka 2012 pamoja na kuweka mikakati ya
namna ya kuendelea kudhibiti na kukabiliana na vitendo vya uhalifu hapa
nchini.
Bi. Senso alisema katika
mkutano huo, mada mbalimbali zitatolewa na wadau kutoka ndani na nje ya Jeshi la
Polisi ambazo zitalenga kuimarisha uwezo wa namna ya kuzuia, kupambana na
kutanzua uhalifu hapa nchini kuanzia ngazi ya familia.
“Mkutano huo unatarajiwa
kuhudhuriwa na mawaziri mbalimbali akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhe. Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Waziri wa
Fedha, Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi, Waziri
wa Kazi na Ajira, Waziri wa Maliasili na Utalii, Waziri wa Kilito, Chakula na
Ushirika, Waziri wa Ardhi na Makazi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Tamisemi, Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Mifugo na Uvuvi pamoja na Waziri
wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto” Alisema Bi.
Senso.
Kauli mbiu katika mkutano
huo ni “Tujenge uwezo wa jamii na Polisi kukabiliana na vurugu kwa kuimarisha
utii wa sheria bila shuruti
Post a Comment