Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RC TANGA AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI

viewer 4301b
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RC TANGA AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI KUZUNGUMZIA AMANI
Mkuu wa mkoa Tanga Mh. Chiku Gallawa amekutana na viongozi wa dini mbalimbali leo tarehe
21/02/2013 mjini Tanga kwa lengo la kusisitizia umuhimu wa kuwakumbusha waumini na wafuasi
wa dini zao kudumisha amani na kuachana na dhana ya ubaguzi wa kidini. Mazungumzo hayo
yamefanyika ikiwa ni pamoja na kutaka kufahamu ni nini hasa wananchi wanahitaji serikali ikifanyike
ili amani izidi kujengeka .

Akisisitiza hoja yake, Mhe. Gallawa amesema kuwa si muda muafaka kwa wananchi kuendelea
kuilaumu serikali juu ya yale ambayo yanatokea bali wote kwa pamoja lengo liwe ni kuwajibika kwani
serikali ni watu na watu wenyewe ni wananchi wote.

” Umefika wakati wa sisi wananchi kuelewa kuwa kila mwananchi katika mkoa wake ana wajibu wa
kufanya katika kudumisha amani, si jambo la busara kukaa pembeni na kuisonda serikali kidole bali
kushirikiana kwa pamoja kwa umoja wa kindugu kwa faida ya mkoa na taifa letu kwa ujumla. Wote
tujifunze tuvumiliana na kuchukuliana kila mmoja na mapungufu yake”

Aidha wakitoa maoni yao juu ya nini serikali ifanye katika suala zima la amani, viongozi wa dini
wamesema kuwa serikali haina budi kuchukua jukumu la kuielimisha jamii maana halisi ya amani na
umuhimu wake kwa taifa. Pia wamewaasa wananchi kuwa na nia ya kweli na kurudi kwenye maadili
mema.

Kwa upande mwingine serikali imeshauriwa kufanya uchunguzi wa kina kubaini kikundi chochote
ambacho kinaonekekana kuwa chanzo cha uchochezi wa vurugu na kukichukulia hatua kali. Hali hii
itaondoa wasiwasi na woga mkubwa ambao umetanda miongoni mwa wananchi na viongozi wa dini
kwa ujumla.

Vilevile viongozi wa dini wamevikumbusha vyombo vya habari kutokuwa chanzo cha kuchochea
vurugu kwa kutoa taarifa zinazoamsha hisia za chuki miongoni mwa waumini wenye imani tofauti
badala yake kuwa ni vyanzo vizuri ya kudumisha amani.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top