Nje ya Jumba la Somerset- Samson Soboye (Mpangaji wa maonyesho), Jacqueline Kibacha ("Heart 365"), Mama Balozi Joyce Kallaghe, Anna Lukindo ("Anna Luks") na Rose Kiondo (Mratibu wa maonyesho)
Wanamitindo wa Kitanzania kwenye London Fashion Week 2013. Anna Lukindo, Christine Mhando, Jacquiline Kibacha-pic by Urban Pulse"
Jumapili mchana wilaya ya Westminster jijini London ilikuwa na mashindano ya ubunifu na urembo katika maonyesho ya kimataifa ya London Fashion Week. Mashindano haya yalifanyika jumba la Somerset lililosimama imara kwenye upembe wa kaskazi ya mto Thames.
toka tarehe 14 hadi tarehe 28. Wiki hizi mbili nzima zitakutanisha kila mtu anaye husika na biashara ya mavazi na urembo. Magwiji na mapapa wa mitindo, wabunifu, walimbwende, watafuta vipaji, wafanya biashara, wazalishaji mali ghafi na wamiliki viwanda. Wote hukutana katika maonyesho haya. Hapa si vipaji tu vinavyojionyesha, bali pia watu wa biashara.
Siku hii Tanzania ilikuwa moja ya nchi mbili tu za Kiafrika zilizochaguliwa na British Council na "London Fashion Week" kushiriki mashindano ya kutafuta vipaji chipukizi kwenye tasnia ya ubunifu wa mavazi na urembo. Watanzania Anna Lukindo, Jacqueline Kibacha na Christine Mhando ndio wasanii waliobeba bendera ya taifa letu na kutuwakilisha katika mashindano haya ya kimataifa yanayofanyika kila mwaka kwa zaidi ya miaka 27 sas
Post a Comment