UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA ZILIZOTOLEWA
KWENYE VYOMBO VYA HABARI NA MITANDAO JUU YA KUINGIZWA NA KUWEPO KWA DAWA BANDIA
ZA KUTIBU KIFUA KIKUU
<!--[if !supportLists]-->1. Hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari hapa
nchini na mitandao ya kimataifa imetoa taarifa juu ya kuingizwa au kuwepo kwa
dawa za kutibu ugonjwa wa kifua kikuu (Tuberculosis – TB) zinazohisiwa kuwa ni
bandia katika baadhi ya nchi za bara la Afrika ikiwemo Tanzania.
<!--[if !supportLists]-->2. Taarifa zilizotolewa zimeainisha kuwa sampuli
zilichukuliwa kutoka kwenye maduka ya dawa binafsi (private pharmacies).
Ufafanuzi unatolewa kwamba, dawa za TB huingizwa nchini kwa utaratibu maalum
ambapo ni Bohari ya Dawa (MSD) pekee ndiyo hununua na kusambaza dawa hizi katika
vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali na baadhi ya vituo binafsi chini
ya kibali na usimamizi maalum. Dawa zinazoruhusiwa kuingia nchini ni zile
zilizosajiliwa na kuthibitishwa na TFDA. Dawa za kutibu TB haziruhusiwi kuuzwa
kwenye maduka ya dawa binafsi.
<!--[if !supportLists]-->3. <!--[endif]-->TFDA inapenda kutoa
ufafanuzi kwa umma kuwa taarifa hizo sio za kweli. Hii ni kutokana na ukweli
kwamba mifumo ya ufuatiliaji wa ubora na usalama wa dawa ingeweza kubaini dawa
hizo katika soko. Kwa mfano, kwa mujibu wa takwimu zilizopo, matoleo (batches)
89 ya dawa za TB yaliyochukuliwa kwenye vituo vya forodha (ports of entry) kati
ya Januari 2011 na Disemba 2012 na kupimwa kwenye Maabara ya TFDA yameonesha
kukidhi vipimo vya Maabara. Aidha, matoleo 46 ya dawa za TB yaliyochukuliwa
kutoka katika vituo vya afya vya Serikali kati ya Juni – Disemba 2012 pia
yamekidhi vipimo vya Maabara baada ya kuchunguzwa.
<!--[if !supportLists]-->4. <!--[endif]-->TFDA imeweka mifumo thabiti
ya kusajili, kukagua, kuchunguza kwenye Maabara na kufuatilia ubora wa dawa
zilizoko kwenye soko. Kupitia mifumo hii, TFDA inaweza kubaini uwepo wa dawa
duni na bandia katika soko. Pamoja na mifumo iliyopo, TFDA inawaomba wananchi
kutoa taarifa pale wanapokuwa na mashaka kuhusu ubora na usalama wa dawa za TB
pamoja na dawa nyingine ili hatua stahili zichukuliwe kwa mujibu wa sheria.
<!--[if !supportLists]-->5. <!--[endif]-->Mamlaka inawashauri
wagonjwa wa TB kuendelea kutumia dawa za kutibu ugonjwa huo zinazotolewa bure
kwenye vituo vya afya vilivyoruhusiwa na Serikali kwa kuwa ni bora, salama na
zenye ufanisi uliothibitishwa na TFDA.
<!--[if !supportLists]-->6. <!--[endif]-->TFDA itaendelea kufuatilia
taarifa hizo na kufanya ukaguzi zaidi ili kuhakikisha kwamba dawa za TB
zinazotumika nchini ni bora na salama wakati wote.
Kwa maelezo au ufafanuzi
zaidi, tafadhali wasiliana na;
Mkurugenzi
Mkuu
Mamlaka ya Chakula na Dawa
(TFDA),
S.L.P 77150, Dar Es
Salaam
Simu: +255 22 2452108/22
2450512
Au: 0658 445222/ 0685 701735/
0777 700002
Nukushi: +255 22
2450793
Barua
pepe: info@tfda.or.tz, Tovuti:
www.tfda.or.tz
Post a Comment