BAADHI
YA WAANDISHI WA HABARI WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA TAMKO HILO
TANZANIA CHRISTIAN FORUM (TCF) MKOA WA
MBEYA
TAMKO RASMI KUTOKA KTK JUKWAA LA WAKRISTO MKOA
WA MBEYA
MHESHIMIWA NDG. ABAS KANDORO,
KAMA MKUU WA MKOA NA MWAKILISHI
WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE MKOA
WA MBEYA, TUNAPENDA KUSOMA MBELE YAKO TAMKO RASMI LA JUKWAA LA WAKRISTO MKOA WA
MBEYA (TCF).
NDUGU MKUU WA
MKOA,
“HAKI HUINUA TAIFA BALI DHAMBI NI AIBU YA WATU
WOWOTE” (Mit. 14:34).
Katika mkutano wa jukwaa la
Wakristo Tanzania mkoa wa mbeya ulionyika tarehe 12/02/2013 Jijini Mbeya,
wajumbe tulitafakari kwa undani juu ya hali inayoendelea kujitokeza katika nchi
yetu na hasa katika mahusiano baina ya dini mbili kuu UKRISTO NA
UISLAMU.
Jukwaa hilo lilijumuisha
taasisi zake kuu (yaani mabaraza ya Madhehebu ya Kikristo)
Tanzania Episcopal Council
(TEC), Christian Council of Tanzania (CCT) na Pentecostal Council of Tanzania
(PCT).Mbali na mambo yake ya kawaida jukwaa hilo lilitafakari utekelezaji wa
Serikali juu ya tamko Rasmi la jukwaa la Wakristo kitaifa lililotolewa tarehe
06/12/2012 na kusomwa katika makanisa yote ya Kikristo nchini kwenye sikukuu ya
Krismas tarehe 25/12/2012. Katika tafakari letu jukwaa la Wakristo wa Mkoa wa
Mbeya tumeona kuwa kunabaadhi ya mienendo inayojitokeza katika nchi yetu ambayo
kama isipodhibitiwa na kukomeshwa na Serikali italeta athali kubwa na hata
kuondoa amani na uthabiti (Stability) wan chi.
Katika kutafakari kwa jukwaa
juu ya athari zinazoweza kujitokeza, kumekuwepo na mambo yanayotendeka waziwazi
yenye athri kubwa kwa amani na usitawi wan chi na wanchi wake kwa ujumla. Kwa
mfano, uchochezi, kashfa, matusi na uchokozi wa wazi unaofanywa na baadhi ya
waumini wa dini ya Kiislamu kupitia vyombo vya habari vya kidini (rediona
magazeti), mihadhara, kanda za video, CD na DVD pamoja na kauli zinazotolewa na
viongozi wa dini hiyo kwenye baadhi ya nyumba zao za ibada(ushahidi upo kama
vile uhamasishaji wa Sheikh Ilunga) pasipo serikali kuchukua hatua stahiki na
badala yake kubaki kimya au kupambana na wanaofichua harakati hatarishi kwa
utulivuwa nchi.
Miongoni mwa harakati hatarishi
zinazosambazwa kwa njia ya CD na DVD za Sheikh Ilunga, kuhusu kuua Wachungaji,
Mapadri na Maaskofu zimeanza kuwa matokeo mabaya; kwani Padri kule Zanzibar
alipigwa risasi na watu walioitwa na serikali wahuni na sasa
kifo
Kimetokea na mchungaji Mathayo
Kachila kule Buselesele Mkoani Geita na kikundi kinacho dhaminiwa ni
wanaharakati hao wa kiislamu wenye jazba na gadhabu kali inayotokana na mvutano
uliopo kati ya wakristo na waislamu kuhusu nani mwenye haki kisheria KUCHINJA
WANYAMA. Hatua zinazochukuliwa na Serikali hazilizishi wala kukidhi matakwa ya
wananchi wapenda amani. Tuna mifano kadhaa ya matukio kama haya yaliyojitokeza
kwa wanchi wenzetu moja ni ile ya wenzetu aliyepigwa risasi kule Rungwe Ndg.
John Mwankenja (Mwenyekiti wa CCM Rungwe) aliyepigwa risasi kwa mambo
yanayodhaniwa kuwa ni ya kisiasa) Serikali ichukuwe hatua madhubuti kwa kutuma
wachunguzi kutoka Dar es salaam kwa swala hilo na wote tuliridhika kwa hatua
hizo madhubuti. Hatua kama hizo mbona hazichukuliwi katika masuala haya ya
kidini na badala yake Serikali inakaa kimya au ina chukua hatua ambazo kimsingi
hazitatui tatizo ili wananchi waridhike na Seeikali yao? Je tuseme Serikali
inaangalia haiba (Personality) za watu au aina ya vikundi? Swala la uchinjaji
lilipo jitokeza kule Mwanza waziri wan chi ndg. Steven Wasira alienda na kutoa
majibu mepesi katika swala zito je, tuseme aliyoyatamka huko yalikuwa ni KAULI
YA SERIKALI au kauli yake mwenyewe? Na kama yake mwenyewe mbona Serikali
haijakanusha waziwazi? Na kama ni kauli ya serikali hiyo haki ya kuchinja kwa
waislamu inatokana na sheria zipi za nchi? Je huo ndio utawala wa sheria
tuliyoahidiwa na serikali ya awamu ya nne kuwa itatenda kazi kwa kuzingatia
utawala wa sheria.
Kupigwa risasi kwa Pdri na
kuuwawa kwa mchungaji kunathibitisha hazma halamu na batili ya “Ua, chinja”
mapadri, wachungaji na maaskofu iwe kwa siri au kwa wazi iliyohasisiwa na Sheikh
Ilunga ambayo sio tu inahatarisha amani ya nchi lakini pia inavunja haki za
kuishi za binadamu zilizoainishwa katika katiba ya serikali ya jamuhuri ya
muungano wa Tanzania. Aidha harakati hizi ziana muelekeo wa kudhoofisha ukristo
Tanzania kama sio kuumaliza kabisa. Pamoja na mambo mengine kinachosikitisha ni
namna ambavyo serikali inavyoyashughulikia mambo mazito yanayotikisa amani na
utulivu wan chi. Utasikia mala ikisema “Mtu haruhusiwi kujichukulia sheria
mkononi” na ndipo kikundi Fulani kitaibuaka na kuvunja mabucha na kuchoma nyama
iliyomo humo hapo tena utasikia serikali hiyohiyo ikitowa kauli kwamba
“Mvumiliane” je tunakwenda wapi?
Kwa misingi hiyo kwanini tusite
kusema kwamba serikali ya chama cha mapinduzi (CCM) inaibeba dini ya kiislamu?
Kwakuwa jukumu la serikali ya chama cha mapinduzi ni kuhakikisha kuwa wananchi
wote wa Tanzania bila kujali dini zao, makabila yao na hata rangi zao wanaishi
katika misingi ya uhuru, haki, udugu na amani kama raisin a watendaji wake
walivyotoa kiapo mara baada ya kupewa dhamana ya kuiongoza nchi na wananchi wake
kwa ujumla pasipo na ubaguzi wowote.
HITIMISHO: Ili wakristo wote
nchini warudishe imani yao kwa serikali ya chama cha mapinduzi mambo ya fuatayo
ni lazima yachukuliwe hatua za haraka iwezekanavyo:
- Tunataka Serikali izingatie utawala washeria kulingana na ahadi
yake katika kushughulikia maswala ya kijamii na sio vinginevyo. Kwa kuzingatia
sheria maswala ya imani na dini yapo wazi kabisa kama zilivyoanishwa kwenye
katiba ibara ya 19 (1), (2) (3) (4) na kufanya vinginevyo ni uvunjifu wa
sheria.
- Swala la kuua lisichukuliwe kama mazoea ya kawaida na inapotokea
popote ni lazima Serikali ichukuwe hatua inayostahiki kwa kuzingatia utawala wa
sheria kwakuwa wote wako sawa mbele ya sheria ibara ya 12, 13 (1) –(5).Usawa huo
ni lazima uonekane katika swala la mauaji ya Mchungaji Mathayo Kachila na kama
hatua zilivyochukuliwa katika mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri na
mwenyekiti ya CCM Wilaya ya Rungwe Ndg. John A. Mwankenja. Hiyo ni haki ya
msingi kkwa kila mtantania bila kuangali haiba (Personality) yake kama katiba ya
Jamuhuri ya muungano wa Tanzania inavyoainisha haki xza kuishi, kulindwa na
kushughuklikiwa kisheria katika ibara ya 14 na 15 pamoja na vifungu vyake viwili
vidogo.
- Tunataka Serikali itueleze ni ushahidi gain zaidi inayoutaka
kuliko ule unaopatikana kwenye CD na DVD zilizotolewa na Sheikh Ilunga kama
inazingatia utawala utawala wa sheria.
- Tunataka Serikali iwajibike kutolea ufafanuzi kauli ya waziri
wan chi Ndg. Steven Wasira inayohusu haki ya kuchicha kwa waislamu kama
inatokana na sheria gain ya nchi?
- Kama Serikali inatekeleza utawala wa sheria, tunataka wakristo
tuwe na machinjio na bucha zetu kulingana na imani yetu.
- Kama Serikali haitachukuwa hatua za makusudi katika kutekeleza
madai yetu sisi kama viongovi wa dini ya kikristo tutachukua hatua ya kuwaambia
waumini wetu kwamba Serikali ya chama cha mapinduzi inaibeba dini ya kiislamu na
wao watajua la kufanya.
Pamoja na kutaka utekelezaji wa
haraka kutoka kwa Serikali bado tunawaomba wakristo tuwe katika hali ya maombi
na utulivu kwa wakati huu ambapo tumo katika vita vya kiroho ili Mungu
akatuimarishie amani ambayo ni nguzo kuu ya Taifa letu. Tamko hili rasmi la
jukwaa la wakristo Mbeya lisomwe katika makanisa yetu yote siku ya juma pili
tarehe 24/02/2013.
Tunakuambatanishia na nakala ya Tamko Rasmi la TCF Taifa la
tarehe 6/12/2012.
NDUGU MKUU WA MKOA NAWASILISHA.
Nakala kwa:
- Mwenyekiti wa CCM Mkoa.
- Tanzania Christian Furum Taifa
- Mwenyekiti wa the Tanganyika Law Society.
- Vyombo vya habari TV, Redio na magazeti
Post a Comment