Na Mahmoud
Ahmad,Arusha
TANZANIA imepata tuzo tatu za maajabu saba ya
Afrika kupitia vivutio vyake bora vya utalii vya Mlima Kilimanjaro,Hifadhi ya
Ngorongoro na Hifadhi ya Serengeti ambayo ndio iliongoza kwa kupata kura nyingi
kuliko nchi nyingine yeyote.
Akitangaza matokeo hayo
jana mjini hapa rais wa taasisi iliyoandaa tuzo hiyo Dk. Phillip Imler wa
Marekani mbele ya waziri mkuu Mizengo Pinda alisema sababu iliyopelekea Tanzania
kupata ushindi huo ni kutokana na kuwa na vivutio vya
kipekee.
Akielezea hifadhi ya taifa
ya Serengeti alisema kuwa ndio hifadhi ya kipekee iliyopata kura nyingi na
kutokana na tabia za misafara ya wanyama wanaohama kwa msimu maarufu kama annul
animal migration.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda,
aliyekuwa mgeni rasmi katika ghafla hiyo, alisema kuwa nchi za Afrika zina
vivutio vingi vya utalii na fursa kubwa ya kukuza pato kupitia utalii
huo.
Alisema kutokana na sifa
ambayo Tanzania imezipata kupitia vivutio vyake vitatu itaendelea kuvitunza
kuhakikisha kuwa vinavutia zaidi watalii na kuongeza pato la
taifa.
“Afrika ina vivutio
vingi vyenye kuvutia hivyo kila nchi ni lazima ijivunie rasilimali hizo kwa
kuvitunza na kuviendeleza,”alisema
“Kwa Tanzania ni bahati ya
pekee kwa kuweza kupata tuzo tatu za maajabu saba ya Afrika ambazo ni za Mlima
Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro pamoja na hifadhi ya Taifa ya Serengeti hivyo
ni wajibu wa kuvitunza na kuviendeleza,”alisema Pinda.
Aliongezea kuwa iwapo
watanzania wataendeleza tabia ya utunzaji wa vivutio vilivyopo nchini, nchi
itaendelea kupata sifa duniani kote.
Naye Mkurugenzi wa Hifadhi
za Taifa,(TANAPA),Dkt. Alan Kijazi alisema mlima Kilimanjaro ni mlima mrefu
barani Afrika na hivyo una kila sababu ya kushinda na watanzania waendelee
kuutunza.
Dkt Kijazi alisema kuwa
hifadhi hiyo imeshinda kwa kuwa kuwa na wanyama wa kila aina kama Big Seven,
Simba, tembo, Viboko, Nyati, Vifaru, Sokwe na Mamba.
Mbali na Tanzania Dk.Imler
alivitaja vivutio vingine vilivyoshinda kuwa ni Red sea Reefs, Okavango Inland
delta iliyopo nchini Botwasana, Sahara Desert na River
Nile.
Aidha Waziri wa Maliasili
na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki alisema ushindi huo ni historia kubwa duniani
na kwamba ni jambo la watanzania wote kujivunia.
Pia aliwashukuru wananchi walioshiriki katika mchakato mzima wa kupiga kura na kuviwezesha kuingia katika ushindi kwa mara tatu.
Pia aliwashukuru wananchi walioshiriki katika mchakato mzima wa kupiga kura na kuviwezesha kuingia katika ushindi kwa mara tatu.
Post a Comment