Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TIBA YA MALARIA YAGUNDULIKA

Nembo-ya-Taifa


Utangulizi
Kumekuwepo na taarifa kupitia baadhi ya vyombo vya habari kwamba kuna upungufu mkubwa wa dawa mseto za kutibu malaria aina ya ALU katika vituo vya kutolea huduma za afya hapa nchini.Taarifa hizo zilimnukuu Mkurugenzi wa shirika lisilo la serikali la SIKIKA, katika mkutano na wahariri wa vyombo vya habari uliofanyika mjini Dar es Salaam hivi karibuni.
Ufafanuzi
Taarifa alizotoa Mkurugenzi wa SIKIKA, chanzo chake kimetokana na kunukuu taarifa zinazopatikana kutoka katika mfumo wa kielektroniki wa wizara ambao unafuatilia takwimu za dawa za malaria katika vituo vya huduma ujulikanao kama ‘SMS for Life’.
Mfumo huu unatoa taarifa za upatikanaji wa dawa za kutibu malaria aina mbili tu ambazo ni Alu na Quinine, na sio dawa nyingine za kutibu Malaria.
Hivyo basi, dawa zingine zote pamoja na zile za msaada, ambazo zinapokelewa na kusambazwa katika hospitali zote nchini hazitolewi taarifa kwa kutumia mfumo huu wa “SMS for Life”. Hivyo kusababisha wakati mwingine kuonekana hakuna dawa wakati dawa hizo zipo vituoni.
Hali halisi
Dawa za Alu zilizopokelewa mwezi Januari 2013;-
  • Vidonge vya watoto dozi 2,400,000 ambazo zitatosheleza kwa miezi 5
  • Vidonge vya watu wazima dozi 5,688,720 zinatosheleza matumizi ya miezi 14
Shehena nyingine za dawa za Alu zinatarajiwa kufika nchini mwezi Machi, 2013.
Aidha, kufikia tarehe 31 Disemba 2012 kulikuwa na dawa za Alu za watoto dozi 1,315,967 ambazo zilitosha matumizi ya miezi 2. Vile vile, kulikuwa na dozi za Alu 2,283,610 za watu wazima ambazo zinatosha matumizi ya miezi 2 na nusu.
Hitimisho
Wizara inapenda kuwahakikishia wananchi kwamba kwa sasa kuna dawa za kutibu malaria vituoni za kutosha. Vile vile, Bohari kuu ya Dawa (MSD) inaendelea na usambazaji wa dawa hizi katika vituo vyote nchini. Aidha, taratibu za kuagiza na kuleta shehena zaidi ya dawa za malaria kutoka nje ya nchi zinaendelea ili kuhakikisha kuwa dawa za kutibu malaria zinapatikana kwa muda wote.
Regina L. Kikuli
KAIMU KATIBU MKUU
01/02/2013
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top