Uchaguzi
wa viongozi wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) unafanyika
Februari 14 mwaka huu mjini Morogoro kama ulivyopangwa, tofauti na taarifa
wanazopewa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho.
Kwa
mujibu wa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya FRAT, Damas Ndumbaro, wajumbe wa
Mkutano Mkuu wa FRAT wanatakiwa kufika Morogoro keshokutwa (Februari 12 mwaka
huu) . Pia wapiga kura na wagombea wanatakiwa kulipia ada za uanachama kwa mwaka
2013 kabla ya uchaguzi.
Wagombea
ni Army Sentimea na Said Nassoro (uenyekiti) wakati wanaoomba nafasi ya Makamu
Mwenyekiti ni Juma Chaponda, Juma Mpuya na Tifika
Kambimtoni.
Abdallah
Mitole, Charles Ndagala na Hamis Kisiwa wanawania ukatibu mkuu, nafasi ya
Mhazini inagombewa na Jovin Ndimbo. Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni Kamwaga Tambwe wakati nafasi ya uwakilishi
wanawake yupo Isabela Kapera.
Wagombea
wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Emmanuel Chaula na Samson
Mkotya.
Post a Comment