1. Kamati ya Uchaguzi ya
TFF imepitia mchekato mzima we uchaguzi we Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) na Uchaguzi wa Tanzania Premier League Board (TPL Board) ili kujiridhisha
kuwa mchaketo mzima wa uchaguzi unakidhi kikamilifu matakwa ya Kanuni za
Uchaguzì na Katiba ya TTF. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imebaini kuwa kuna matatizo
ya kikanuni ambayo yanapaswa kuzingatiwa kwemza kabla ya kuendelea na mchakato
wa uchaguzi.
2. Kamati ya Uchaguzi ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania kwa mamlaka iliyonayo kwa mujibu wa Ibara
ya 10(5) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF INASITISHA zoezi la uchaguzi wa Tanzania
Premier League Board (TPL Board) na Uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) hadi hapo matatizo hayo ya kikanuni yatakapopata
utatuzi.
3. Kamati ya Uchaguzi
itawatangazia baadae tarehe mpya za uchaguzi wa
Tanzania Premier League
Board (TPL Board) na Shirikisho la Mpira we Miguu Tanzania
(TFF).
Deogratias
Lyatto
MWENYEKITI
KAMATI YA UCHAGUZI
TFF
Post a Comment