Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa
mkono wa pole na kuwafariji ndugu, jamaa na marafiki wa familia
zilizoondokewa na watoto na wazazi wao kufuatia ajali ya barabarani
iliyotokea maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa
Pwani Februari 11, 2013 iliyoua hapohapo watu wanane wakiwemo wanafunzi
wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark
II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akiangalia moja ya picha za ajali hiyo alizopewa na wanafamilia
walioondokewa na watoto na wazazi wao kufuatia ajali ya barabarani
iliyotokea maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa
Pwani Februari 11, 2013 iliyoua hapohapo watu wanane wakiwemo wanafunzi
wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark
II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na lori
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akifariji ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto
na wazazi wao kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea maeneo ya kijiji
cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani Februari 11, 2013 iliyoua
hapohapo watu wanane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya
Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II lililokuwa limebeba
abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli.
Haya ndio magari yaliyopata ajali
hiyo na kupelekea vifo vya watu wanane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya
Sekondari ya Chalinze.PICHA NA IKULU.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete Jumamosi hii ya Februari 16, 2015 amekwenda
kuhani na kufariji ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa na
watoto na wazazi kufuatia ajali ya barabarani maeneo ya kijiji cha
Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani iliyotokea Februari 11, 2013
na kupoteza hapohapo maisha ya watu nane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya
Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II
lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli la
mizigo.
Familia
alizokwenda kuhani na kuzifariji ni pamoja na za marehemu Hassan Erasto
Kurunge (57), Maria Sadiki ((52) na mtoto wa mwaka mmoja Samweli
Ismail wa kata ya Ubena.
Wengie ni marehemu Essau Enos Mwamgingo (16) , Stella Isaack Kazimoto (18), Bahati George Mbena (17) na Latifa Maneno (17).
Akiwa
ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Mwantumu Mahiza na Mkuu wa
Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Ahmed Kipozi, Rais Kikwete alieleza kusikitishwa
kwake kwa ajali hiyo, na kuwataka madereva wawe makini katika
kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Rais
Kikwete alisikitishwa zaidi kwa taarifa kwamba gari hilo dogo lilikuwa
limebeba abiria wanane, na kuwa dereva wake ambaye pia alipoteza
maisha, hakuwa makini katika kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Post a Comment