“Athman Nyamlani Mgombea
Urais Pekee wa TFF mwenye vigezo kuliko wagombea wote”
KUSITISHA ZOEZI LA
KAMPENI
12/02/2013
1. Kamati ya Uchaguzi, kwa
mamlaka iliyonayo kupitia Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 3(1), 6(1) (g) na
(l), 10(5), 11(6) inayosomeka pamoja na Ibara ya 14(1) na (2) na pia Ibara ya
26(5) na (6), imesitisha zoezi la kampeni za uchaguzi wa TFF na TPL Board
lililokuwa lianze kesho tarehe 13/02/2013 hadi hapo itakapowatangazia, ili
kuhakikisha kuwa mchakato wa uchaguzi unakidhi kikamilifu matakwa ya Kanuni za
Uchaguzi na Katiba ya TFF.
2. Tarehe za Uchaguzi Mkuu
wa TFF na TPL Board zinabaki kama zilivyopangwa.
3. Taarifa hii inazingatia
pia Ibara ya 2(4) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF inayoagiza uongozi uliopo
madarakani kuendelea na kutekeleza majukumu ya Shirikisho hadi hapo mchakato wa
uchaguzi utakapokamilika.
Deogratias
Lyatto
MWENYEKITI
KAMATI YA UCHAGUZI
TFF
Post a Comment