Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, PEREIRA AME SILIMA AWAPA SOMO MAAFISA MAGEREZA NCHINI KATIKA MAFUNZO YA JINSIA AWAMU YA PILI.

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akimsalimia Mwezeshaji wa Mafunzo ya Jinsia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Asina Omari (kulia) kabla ya kufungua mafunzo ya Jinsia awamu ya pili mjini Morogoro leo. Kushoto ni Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa. Pereira aliwataka maafisa wa jeshi hilo wahakikishe msongamano ndani ya magereza nchini unapungua.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima ili afungue mafunzo ya jinsia kwa maafisa hao.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akizungumza na maafisa mbalimbali wa jeshi la magereza kabla ya kufungua mafunzo ya jinsia kwa maafisa hao.
Maafisa Magereza wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Pereira Ame Silima (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya jinsia mjini Morogoro.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (wa katikati waliokaa) akiwa na Viongozi watendaji, maafisa wa Jeshi la Magereza, wawezeshaji wa mafunzo ya Jinsia, na watumishi raia wa jeshi hilo katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi mafunzo hayo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top