Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (katikati) akikata utepe kwa kushirikiana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki Duniani Yukiya Amano (wa pili kutoka kushoto) kuashiria uzinduzi rasmi wa jengo jipya lenye vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa kansa katika Taasisi ya Kansa leo Ocean Road jijini Dar es salaam. Wengine ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto), Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kansa Ocen Road Prof. Twalib Ngoma (wa tatu kutoka kushoto) na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid.
Waziri
mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (katikati) akiwaonyesha wageni mbalimbali
waliohudhuria uzinduzi wa jengo jipya la kuwahudumia wagonjwa wa kansa katika
Hospitali ya Kansa Ocean Road kitabu cha Mkakati wa Kitaifa wa Kudhibiti na
kupambana na Kansa nchini.
Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini
Dar es salaam mara baada ya kuzindua jengo jipya la Taasisi ya Kansa Ocean Road
lililojengwa na serikali ya Tanzania lenye uwezo wa kuhudumia wa 257 kwa gharama
ya shilingi bilioni 7.2 huku Shirika la nguvu za Atomiki Duniani (IAEA)
likichangia mashine 2 za kutambua sehemu zilizoathiriwa na ugonjwa wa kansa
katika mwili wa binadamu zenye uwezo wa kuhudumia wagonjwa 1600 kila moja kwa
mwaka.
Baadhi
ya wataalam wa Taasisi ya Kansa ya Ocean Road wakiwa ndani ya moja ya chumba
cha jengo jipya lililozinduliwa jijini Dar es salaam chenye moja ya mashine
yenye uwezo wa kuwahudumia wagonjwa 1600 kwa mwaka. Mashine hiyo imetolewa na
Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA).
Sehemu
ya nje ya jengo jipya la Taasisi ya Kansa ya Ocean Road lenye vifaa vya kisasa
lilozinduliwa leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
mkuu wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki Duniani Yukiya Amano
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es salaam mara
baada ya kuzinduliwa kwa jengo jipya la Taasisi ya Kansa Ocean Road lililojengwa
na serikali ya Tanzania huku shirika hilo likitoa msaada wa mashine mbili kwa
za kutambua athari za ugonjwa wa kansa kwenye mwili wa
binadamu.
Post a Comment