Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Mazingira Mh. Dkt. Terezya Huviza akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika kiwanda cha bia cha
Serengeti, ambapo amesema kutokana na hali alioiona pale, itabidi kwanza
kuwashirikisha NEMC na kuona jinsi gani watashauriana na kama itabidi kukifunga
itabidi aondoe hati ya mazingira kisha kukifunga kiwanda
hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Mazingira Mh. Dkt. Terezya Huviza leo ameendelea kufanya ziara za
kushtukiza katika viwanda na mahoteli mbalimbali jijini Dar es salaam kuangalia
hali ya usafi wa mazingira.
Katika ziara hiyo Mh waziri
na ujumbe wake wametembelea kiwanda cha Bia cha Serengeti, CI Group Marketing
Solution, Coco Beach, hoteli za Golden Tulip na Sea Cliff.
Akitoa maamuzi kuhusu
mazingira aliyoyakuta katika kila sehemu, Mh. Dkt. Huviza amesema Kiwanda cha
Serengeti kina mfereji unaomwaga maji machafu na bahati mbaya unatitirisha
katika makazi ya watu kitu ambacho ni hatari, hivyo atashauriana na NEMC na
Mwanasheria waone jinsi ya kuwasaidia, lakini kama itashindikana kwa kuwa maji
wanayomwaga ni mengi sana itabidi wafunge kwa muda.
Kuhusu maeneo mengine
aliyoyatembelea Mh. Waziri amesema hawezi kutoa maamuzi kwa sasa kwa sababu kila
aliyekutwa na makosa amepewa muda wa kuyarekebisha na ambaye atashindwa kufanya
hivyo basi atafungiwa kwa mujibu wa sheria.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais – Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa akiwasili katika kiwanda cha
bia cha Serengeti Breweries baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika kiwanda
hicho kujionea namna gani wanatunza Mazingira.
Afisa Mazingira wa Kiwanda
cha Serengeti Breweries Dominick Elibariki akitoa maelezo ya namna wanavyotibu
maji taka ya kiwanda hicho kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira
Mh. Dkt. Terezya Huviza aliyeambatana na maafisa kutoka Baraza la Hifadhi ya
Mazingira (NEMC).
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Mazingira Mh. Dkt. Terezya Huviza akiendelea na ukaguzi wa maeneo
mbalimbali ya kiwanda hicho.
Moja ya mtaro unaotiririsha
maji yenye kemikali yanayotoka ndani ya kiwanda cha Kampuni ya Serengeti
Breweries uliolekezwa na kupitisha maji yake yenye harufu kali karibu na makazi
ya watu.
Sehemu ya mtaro wa maji
machafu yanayotoka ndani ya kiwanda cha bia cha Serengeti ambao umesafishwa na
kulundika lundo la uchafu pembezoni mwa ukuta wa nyumba ambayo ni makazi ya
watu.
Mkazi wa Kata ya
Chamwenyewe iliyopo maeneo ya Chang’ombe Bi. Mwaka Washokera akimweleza Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa adha
anayoipata yeye na familia yake kutokana na mtaro wa maji machafu ya kampuni ya
bia ya Serengeti ambao umepita uwani kwake, na kipindi cha mvua kusababisha maji
machafu yenye kemikali kuingia katika nyumba yake.
Mama huyo pia amesema
kampuni hiyo imemnyanyasa kijinsia kwani alikuwa akilima bustani ya Mboga uwani
kwake lakini kutokana na mtaro huo kupita karibu na uani kwake ameshindwa
kuendelea na bustani hiyo amelalamikia pamoja na moshi mzito unaotoka ndani ya
kiwanda hicho na kusababisha watoto kukohoa kila mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais – Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa akiangalia mtaro wa maji
machafu uliopita uani kwenye nyumba ya Mama Mwaka
Washokera.
Afisa Mkuu wa Mazingira
wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bi. Ruth
Lugwisha akichukua sampo ya maji yanayotiririka kutoka katika kiwanda cha
Serengeti Breweries kwa ajili ya vipimo kama yana madhara kwa binadamu ambapo
bomba lake limeelekezwa kwenye makazi ya watu.
Mtaro wa maji yenye
kemikali unaotokea kwenye kiwanda cha CI Group cha uchapishaji kilichopo jirani
na kiwanda cha bia cha Serengeti kilichopo maeneo ya
Chang’ombe.
Mkazi wa Kata ya
Chamwenyewe Bi. Mwamtema akimuonyesha Waziri wa Mazingira Dkt. Therezya Huvisa
adha wanayoipata kutokana na maji yanayotiririka kutoka kwenye viwanda hivyo
ambayo hujaa katika mifereji hiyo na kuingia katika
makazi.
Mmoja wa wafanyakazi wa
kiwanda cha CI Group akimuonyesha Waziri Upande zilipo Ofisi za mabosi wa
kampuni hiyo ambapo katika Mazingira ya kutatanisha walikuwa hawaonekani kiwanda
hapo baada ya Waziri kuingia lakini cha kushangaza magari yao yalikuwa yamepaki
nje ya ofisi hizo kuonyesha kwamba wapo ndani.
Pichani Juu na Chini ni
sehemu ya kupunguza stress wanayotumia wafanyakazi wa kiwanda cha CI Group
wakiwa wameandika ujumbe unaosemeka” Tumechoka na Vyoo” ambapo Mheshimiwa Waziri
aliamua kuingia kukikagua na kujionea hali halisi.
Kumradhi kama picha hii
itakukwaza lakini haya ndio mazingira ya kazi kwenye baadhi ya viwanda vyetu
nchini.
Baadhi ya wafanyakazi wa
kiwanda hicho wakifurahia ujio wa Waziri wa Mazingira wakijua ya kwamba
wataboreshewa mazingira ya kufanyia kazi.
Pichani Juu na Chini Waziri
wa Mazingira Dkt. Therezya Huvisa akikagua mtaro wa maji machafu ya kiwanda
hicho.
Post a Comment